Tuesday, January 11, 2011

MTUME PAULO HAKUA NA NDOA IWEJE AIZUNGUMZIE?

         John Lisu mmoja wa waimbaji maarufu,hapa ni siku ya Ndoa yake mwaka jana mwishoni

Afadhali YESU naweza sema jambo lake linaeleweka maana yeye alikuja kama MUNGU asilimia mia moja na katika mwili asilimia hizo hizo. Alizaliwa si kwa damu na nyama tu kama alivyo mtume Paulo bali na Baba wa mbinguni katika ROHO. Na alikuja maalumu kutafuta Roho zilizopotea (mathayo 18:11). Mtume Paulo anakua tofauti yeye alizaliwa katika mwili tu(Biological birth).
    
Kwa mujibu wa wanatheologia wanadai kwa desturi za wakuu wa dini wa kiyahudi asingeweza kufikia cheo alichofikia bila kua na mke. Hata hivyo baada ya Paulo kuokoka biblia iko kimya haimtaji mke waPaulo hivyo kumyima USHUHUDA wa kutosha kuweza  kuwa mshauri wa ndoa katika mtazamo wa dunia ya leo.
    
Kwa mtazamo wa KIMUNGU Mtume Paulo amekua ndiye mshauri wa ndoa aliyesifika na maelezo yake bado hadi leo yanatumika 1korintho sura ya 7 yote ameeleza sababu za kutovunjika ndoa katika Bwana. Si hapo tu katika vitabu vyake vingine hususani wagalatia na waefeso pia ameeleza.

                
          David Robert Huyu nae ni mwimbaji maarufu,hapa ni siku ya Ndoa yake Mwaka 2010 mwishoni


Kimsingi ROHO MTAKATIFU mwenye uzoefu wa kila kitu ndiye alikua mwalimu mkuu wa Paulo kuliko hata watu walio ndani ya ndoa. Kiwango au viwango vya ROHO mtakatifu alivyotembea navyo Paulo ndivyo vilimfanya aielezee ndoa vizuri kuliko hata watumishi wengine walio ndani ya ndoa.
   
Hatuwezi bisha leo kuna watu wana uzoefu na ushuhuda wa kua na ndoa zao zasiku nyingi, na wamefanya mengi kanisani, lakini pamoja na ushuhuda mzuri walio nao haujawasaidia kumaliza tofauti zao. Hapa kimsingi hatuhitaji kutumia ushuhuda wa uzoefu kama tija ya kuiboresha ndoa, bali zaidi tutumie mwongozo wa ROHO mtakatifu kwa kila jambo. Hii ni kwa kua yeye (ROHO) ni mzoefu na mwenye siri za ndani za kila eneo, yeye maishani abaki kua Mwalimu wetu na sisi tuwe tegemezi kwake
    
Hivyo ushuhuda wa kua na ndoa tu haumuhalalishi kila mwanandoa kua mshauri mzuri wa ndoa, bila ROHO mtakatifu atachoweza kushauri ni basics tu za ndoa kwa kua anaufahamu nazo. ROHO mtaakatifu anabaki kua kinara wa kutufundisha kila kitu na kwa upeo kwa kua ndiye atupashaye habari za sirini na mshauri wetu mkuu (Isaya 9:6).

                           

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...