Sunday, February 20, 2011

FILAMU ZA KITANZANIA NA MAUDHUI YAKE KWA KANISA


Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na mafanikio makubwa kwa soko la filamu hususani zile zitengenezwazo hapa hapa Tanzania. Mtazamo juu ya Filamu hizo umebadilika leo hii sio watoto na wakina mama pekee ndio wanapendao kuziangalia bali wababa na wazee pia wako mstari wa mbele katika hilo. Zipo Filamu nyingi zenye maudhui tofauti tofauti na mwisho wa siku huingizwa sokoni ambako wakristo na wasio wakristo hupata nafasi ya kuzinunua na kuziangalia.
                Ni wazi kua kiimaadili ya kikristo zipo filamu za kuziangalia na zipo za kuzirusha kwenye dust bin.Wakristo wengi hupenda kuangalia filamu kama sehemu ya kupumzika na kure-fresh, sasa tatizo linakuja watapata wapi filamu za Kiswahili zenye mafundisho chanya pasipo kukwazika katikati ya filamu hizo!!!. Kanisa la leo halihitaji filamu kama filamu zenye mafundisho ya ki-mungu pekee bali linahitaji filamu zenye UBORA kuanzia kwa wasanii wenyewe wawe na ushuhuda mzuri mbele ya jamii, Production ya viwango vya juu, Ujumbe sahihi kulingana na Biblia na standards za kikristo pasipo mbwembwe tuzionazo leo kwenye filamu zilizopo kuhusu wokovu.
               Kulingana na kuenea kwa sayansi na Teknolojia kanisa hususani la Tanzania halina budi kuichukulia Tasnia ya Filamu kama mkondo mwingine wa kupeleka injili kwa wanzania wenzetu na nje ya Tanzania. Makanisani waandaliwe vijana sio kufundishwa tu kuigiza bali waandaliwe kifikra kuwa hata uigizaji wa Filamu nao ni utumishi. Kama mtu anaweza akaimba na kuyagusa maisha ya watu kwa utukufu wa Mungu,vile vile muigizaji wa filamu anaweza akaigiza na kuyagusa maisha ya watu kupitia uigizaji kwa utukufu wa MUNGU.
               Kwa wenzetu nje, kanisa imeliona hili ndio maana leo kuna orodha ndefu ya waigizaji waliookoka ambao ni mamilionea, tumeshuhudia nchi za wenzetu makanisa yakianzisha makampuni ya Filamu kwa kua wamegundua Filamu ni mfereji mwingine wa kumpitisha kristo katika maisha ya watu. Lengo hapa sio kufanya Filamu kwa kua wenzetu waliookoka nje wanafanya bali tunafanya kwa kua imetupasa kufanya kama sehemu ya utumishi wetu ndani ya Kristo Yesu. Leo hii kijana anaweza asisome Biblia wala kwenda kanisani Mwezi mzima ila akaangalia filamu zaidi ya tano kwa mwezi huo huo. Japokua kwa sasa Tanzania kuna baadhi ya watumishi wameanza kuliona hilo ila juhudi mathubuti ni lazima zichukuliwe ili kulifanikisha hilo.
Jenifer Mgendi ni miongoni mwa watumishi wa Mungu hapa Tanzania walioamua kuanza kutengeneza Filamu zenye maudhui ya kikristo.Mpaka sasa Mgendi ndiye anayeongoza kwa kutoa filamu nyingi miongoni mwa watumishi hapa Tanzania,ameshatengeneza Filamu tatu na zote ziko sokoni ambazo ni Joto la Roho,Teke la Mama pamoja na Pigo la Faraja.
Haris Kapiga Muimbaji wa nyimbo za injiri,Mc Maarufu jijini Dar-es-salaam,na Mtangazaji wa Clouds FM naye ameanza kushiriki kuigiza katika Filamu na Tamthilia zenye mafundisho ya kikristo
Mchungajii Upendo Kilahiro naye ametengeneza Filamu inayohusu maisha ya ukristo
Sarah Mvungi ni miongoni mwa wasanii toka kundi la Kaole Sanaa Group ambaye kwa sasa anajishughulisha na uigizaji wa Filamu na tamthilia,Mbali na uigizaji Sarah ni Nesi na Muimbaji wa nyimbo za Injili
Bishop TD Jakes chini ya kampuni yake ya TD JAKES Co Ltd amefanikiwa kutengenea Filamu zenye maadili na shuhuda za kikristo. kati ya filamu zilizoipa umaarufu kampuni yake ya Filamu ni Filamu ya Not easly Broken na Woman thou at Loosed iliyochezwa kwa umahili na mwanamama Kimberly Elise.
Askofu Thomas Jakes(TD JAKES) licha ya kumiliki kampuni linalotengeneza Filamu,pia hushiriki kuigiza.Hapo juu ni moja ya vipande alivyoshiriki katika Filamu ya Woman thou at Loosed.Hapo alienda kumtembelea gerezani mwanadada Kimberly Elise
Woman thou art Loosed filamu maarufu iliyotengenezwa na Kampuni ya Filamu inayomilikiwa na askofu TD Jakes
Kama umewahi kuiona hii Filamu utakubaliana na Hosanna Inc kua Haichoshi,inamafundisho ya Kikristo yenye kuvutia,ni moja kati ya kazi toka kwa askofu Td Jakes
Jumping the Broom,Filam mpya chini ya kampuni ya TD Jakes inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 6 mwezi wa Tano mwaka huu wa 2011

Miongoni mwa watumishi wa MUNGU waliofanikiwa katika tasnia ya Filamu Duniani huwezi kuacha kumtaja Tyler Perry Chini ya kampuni yake ya Tyler Perry Co Ltd. Ametengeneza Christians Muvies nyingi huku akiwashirikisha watu maarufu katika filamu hizo.
Tyler Perry mkurugenzi na mmiliki wa Tyler Perry Films Co Ltd
Moja kati Filamu zenye mafundisho ya kikristo zilizotengenezwa na kampuni ya Tyler Perry
Moja kati ya kazi mahiri toka kwa Tyler Perry
                                                                          
                                                                                                                                                     

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...