Tuesday, February 15, 2011

KWA MPENDWA KUFANYA KAZI ZA PROGRAMU ZA KONDOMU IMEKAAJE?

Care International moja kati ya Mashirika yanayofanya kazi ya kuihudumia jamii ikiwa ni pamoja na kugawa mipira ya kiume na kike pindi inapohitajika na jamii husika.

By Edna

Jamani naomba mnisaidie hapa, na yamkini mchango wenu wa mawazo utaweza kunifanya niache au nifanye hiki kitu kwa ujasiri zaidi.
Nimechaguliwa kuwa focal person wa mambo ya AIDS/HIV miezi mitano iliyopita hapa ofisini kwetu, sasa kuna mlokole mwenzangu mmoja alikuja ofisini kwangu akanikuta niko full package kikazi zaidi na full vifaa kuhusu AIDS/HIV yaani vipeperushi, condoms za kumwaga, n.k akaniambia sasa naona umeamua kuwaambia watu wakazini/wauasherati....nikajaribu kumuelewesha nia yangu lakini bado haikuwa rahisi kwake kunielewa. Nikakaa baadae nikaona yamkini mimi ndio nahitaji kueleweshwa ama yeye ndio anahitaji kuelewa kwahiyo nikaamua niliweke hili kwenu wadau .

1. Hivi kuwapa watu condom ni kuwasaidia au kuwafanya waangamie kabisa, what if your intentions ni kuwasaidia maana hao ambao wanapatikana na maambukizi ni hao hao wa makanisani kwetu na misikitini, tunafanyaje ili kuhakikisha tunawasaidia katika hili ili wakianguka waweze kuanguka salama??
Kuna movie inaitwa MADEA GOES TO JAIL kwa wale ambao wameiona, kuna mdada mmoja MKRISTO yaani mimi ningemwita mlokole, anafanya kazi ya kuhubiri wagerezani, kuwahubiria makahaba(na yeye kabla ya kuwa saved alikuwa kahaba) na wanaokubali kubadilika anawasaidia kupata kazi na kuishi nao. Wengine ambao wanaendelea na ukahaba au madawa ya kulevya anapita kwenye magenge yao(mahali ambao wanafanya huo ukahaba na kula unga) na kuwapa sindano za kujidungia ili wasishirikiane sindano kitu ambacho sio afya na madada poa huwapa condoms. Kwa mawazo yangu sikuona shida katika hilo kwa sababu matokeo positive yalikuwa yanaonekana, kweli makahaba walikuwa wanabadilika baada ya muda na walikuwa wanamkubali kweli labda manabii, mitume, mashehe mniambie au na mimi nilikula tango pori-maziwa yaliyogishiwa??
2. Kuna maswala ya uzazi wa mpango pia, ingawa kwa imani nyingine pia hili nalo ni dhambi, lakini pia condom inatumika kwenye uzazi wa mpango.

3. Pia kuna situations, mfano kama mumeoana na wote mkagundulika mna maambukizi ya virusi vya UKIMWI, mnatakiwa mtumie condom ili kusaidia uenezwaji wa virusi kwenu wote wawili na kuzifanya dawa(kwa wale wanaotumia ART) zisiwe resistant. Au hata kama amekutwa mmoja na maambukizi hayo itabidi hiyo couple wawe wanajisavia wka kutumia condom ili msambazwaji wa maambukizi ya virusi usitokee.
Hebu naomba mnisaidie katika hili wapenzi katika bwana maana SHIRIKA langu pia halina dini.


Edna

                                   xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx



Cements

1. Papaa said...
Je tunasemaje Watumishi wa Mungu wanaowataka dada zetu, wake zetu ana Rafiki zetu wa kike? Nadhani suala la kutaka kufanza zinaa haijalishi wewe ni mwansheria ama daktari, ngoja nikupe Biblical Point of View, Daudi alitembea na Bethsheba lakini Daudi si Daktari, Amnoni na Tamari walibakana si Madktari, Sex ni hulka ya mtu.
Embu kwanza tuache malumbano yasiyo na tija mie napenda hoja Kama Edna anachofanya ni Kibaya ni kibaya how, na kama anachofanyani ni sahihi kwa vipi, tuweke hoja mezani, hakuna anayejua wote tunaelimishana mimi ntasema mbaya sababu moja mbili tatu, mie ntasema ni poa sababu a,b and ila uwe mwangalifu on x, y, and z.

2. Protace said...
Nadhani nimefuatilia vizuri. Sioni shida iliyopo juu ya kazi yake.
Nafasi yake ya kazi kuharibu ukristo wake ni jambo ambalo atakuwa amependa mwenyewe. Unaweza kufanya hiyo kazi na bado ukabaki salama.
Kuandika jambo hili kwenye marafiki huru ni kuonyesha ukomavu wa edna na pengine nia ya moyo maana wapo wengi wanaofanya madadu kimya kimya tuu.
Sote tunajua system ya siasa ya nchi. Je vipi addo ukipewa mlungula( kifurushi ) upeleka kwa mtu na mzee presidar katika kampeni za chama. Utafanyaje au haijawahi kutokea?teeeh teeh natania tu mjomba.
Kila kazi ina mazingira ambayo yanaweza kukukosesha mungu so inategemea ni jinsi gani umejipanga.

Kwa mtazamo wangu ni kwamba politics inaweza kukosesha na mungu kuliko hata hizo kazi zinazohusishwa na condom.
Nakumbuka gamanywa alivyoshambuliwa na walokole kwa kuwa mwenyekiti wa tume ya ukimwi.
Tukumbuke kwamba dunia yote ni ya mwovu na sisi tu mali ya bwana na hatuna dunia yetu wenyewe.

Protace 


Kama wa kristo ni jukumu letu kuangaza,Changamoto zinapokuja kwetu hazijakosea mlango,ziko mahali sahihi kwa kua zina masikio ya kusikia kua yuko mtu sahihi wa kukabiliana nazo
                                                             
3. Dr. Lyatuu said...
Waungwana... labda nianze kwa kusema

Lord is good.
Kwa kweli ni faraja na furaha kuona watu wana uhuru wa kutoa mawazo yao kwa kadri bwana anavyo/ alivyowafunulia. Huwa si rahisi kupata platform kama hii ambayo mtu unajisikia kuwa huru kujieleza kwa kadri unavyofahamu bila kuwa na woga wa "kutengwa".
Ni kazi ya Roho wa Mungu kutufundisha namna tunavyoweza kutumia KILA tulichopewa na Mungu - (ikiwa ni pamoja na akili, maarifa na vipawa tulivyopewa), kujipa na kutoa elimu ya kiroho kwa utukufu wa Mungu aliye hai. Wapendwa wengi wameishia pabaya - often kwa kuwa tu wamejikuta wanakabiliwa na situation ambayo kwa namna moja au nyingine hawana jibu sahihi la nini cha kufanya - kuwawezesha kuvuka walipo. Aidha wapendwa wengi wanajikuta "wanalazimika" kuwa katika situation fulani (mfano kufanya kazi kwenye bar), na kwa kuwa wanajua wapendwa kanisani "hawata nielewa", basi wanaamua na kanisani sasa basi. Matokeo ni kujitenga (hakuna anayewatenga... wanajiengua tu wenyewe taratibu. Matokeo ni kwa shetani kuwashughulikia kwa urahisi zaidi - hasa kwa kuwa wapo wapo tu wenyewe. And so... uhuru kama tulio nao hapa MH ni muhimu (na ninaweza kusema ni lazima) ili kukua kiroho. IN essence that is a part of "fellowship" - that is sharing; contributing & receiving from each one of us - jina la Bwana libarikiwe.

4.Mbeki said... 
 
Matumizi ya mipira ya ngono "condom" Kwanza ikumbukwe kwamba hizi ni kinga za "kupunguza" maambukizi ya magonjwa ya ngono na sio kwamba kinga za "kuzuia" maambukizi kwa asilimia 100. Ngoja niwanyambulie: Tafiti za usahihi wa kondomu au kifaa chochote cha kinga kinapimwa takriban kwa njia tatu kubwa yaani Laboratory studies, Epidemiologic studies na kisha/au clinical trials kisha avearge ya takwimu zinapelekea kufanya uamuzi wa kitu tunaita Theoretical and empirical basis of protection. Kwa hiyo ugawaji wa condomu kitafiti ni njia sahihi ya kuwaambia watu kwamba maambukizi ya magonjwa yote ya ngono kwa njia ya maji maji ya uzazi mfno(gonorrhea, chlamydia, trichomoniasis, and HIV na mimba) na ngozi-ngozi (skin to skin) kama (genital herpes, human papillomavirus, syphilis, and chancroid) zinaweza kupunguzwa kwa kiwango fulani kikubwa tu kulinganisha na kutotumia. Hii ni yamini na kweli. Peleka huuu jumbe kwa watumiaji na wala wasidanganywe au kuogopa wakifanya hivi watapunguza uwezo wa kuambukizwa na kuambukiza na watakuwa salama kimwili na kuendelea kusihi na hivyo kuwa taifa la kesho na leo. Inasaidia PERIOD.!! Usahihi wa Condom kwa Mkirsto: Ngono kama ngono nje ya ndoa ni dhambi, iwe salama au si salama. Iwe na kinga au bila kinga, na huu ni ukweli na wala hapa hatuhitaji kudebate. Je ni sahihi kwa Mkristo kugawa au kutoa elimu ya condom kwa watu; je mimi naweza au huwa naotoa: - Jibu ni kwamba mimi nakupa ukweli maana wewe ni mwanadamu, umepewa utashi na unaweza kujua. sikunyimi maarifa ila si-impose imani yangu juu yako. Na mwisho ntakwambia njia sahihi ya kujikinga asilimia mia moja ni kutofanya. wewe uamue. jibu ni kwamba NI SAHIHI kutoa elimu. Mbona tunajifunza juu ya kutengeneza mabomu, kutengeneza pombe, na hata tunajua njia sahihi ambazio tukifanya tunaua wenzetu. Hata wengine tumejifunza judo, karate kia ni nin? je ni vibaya kusoma au kuongelea juu ya mambo haya?? mbona wakristo wengi tu tunamiliki bastola na bunduki eti tunadai ni ulinzi kwani tunajilinda na nini na si tunajua akija mtu uki-shoot unaua...!! sasa kuua si dhambi? kama hutaki kuua bastola ya nini? kwani unawinda mpaka ununue silaha? Kondomu ni kama binduki, kosa ni jinsi unavyoitumia, Kama ni mwenzangu kama Addo umeoa na unahisi hutaki kutumia njia nyingine za uzazi wa mpango, hewala tumia kondomu inakukinga kwa asilimia zake na wala mimba isiyotakiwa kabla ya wakati haitawapateni. Na "discondant pairs" wenye UKIMWI mmoja na mwingine hana ndani ya ndoa tunawapa condomu kibao ili wajikinge kwa ngono salama wasiambukizane ndani ya ndoa. itawaweka salama na kuwasaidia kutunzana na kulea watoto wao wa baadae. CONCLUSION Elimu yoyote ile chini ya jua si dhambi, dhambini matumizi ya elimu hiyo.. kwa aliye na mahitaji ya elimi ya kondomu, uzazi wa mpango, afya na magonjwa kwa ujumla anione kwa muda wake natoa bure au kwa ada/gharama nafuu/kidogo tu. Na hata machapisho na demonstartion waweza kupata pia. kama unahitaji models za kufundishia pia naweza kukuelelekeza wapi pa kuzipata ili Usije ukawadanganya watu kwa maneno mengi wakaelewa visivyo. My human rights jamani   Mbeki
5. Irene said...
Nakumbuka mpendwa mmoja yeye anafanya kazi Breweries tena section ya kuweka chemicals/alcohol ili hizo liquids ziwe pombe kamili... tena anakagua kama zimekolea. Ni mtumishi mzuri na muhubiri/mwalimu wa gospel.
Alichotuambia yeye ni kuwa huwa anapitia mitungi sijui barrels moja moja na kuziombea kuwa wanywaji waokoke, na pia wafanyakazi wa hapo Breweries waokoke.
Anasema there was a wave of revival huko Breweries as a lot of staff were born again.

Sasa hapo pima mwenyewe... hiyo strategy yake it works or not na pia pima mwenyewe kama je ni hii is just a justification ya yeye kufanya kazi huko?
Angalizo ni kuwa some things may not be sin, but may contradict your faith.
It may not be sin, but my compromise your faith - si wote wana ujasiri wa kupona katika maeneo hayo meaning some may end up back sliding, taratiiibu.
May not be sin but may confuse others who would like to come to Jesus or those newly born again....

Kubwa ni kuwa na uhakika ndani yako kuwa where you are is where God wants you to be.... si Breweries tu, popote, anguko halijali ni wapi unafanya kazi.

Irene

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...