Friday, September 16, 2011

Askofu Emmanuel Lazaro wa TAG kufanya Semina ya UREJESHO Living water Centre kwa Ndegi


Askofu Emmanuel Lazaro
Askofu Emmanuel Lazaro wa TAG pamoja na Askofu Moses kulola ni kati ya Maaskofu wanaoheshimika sana nchini Tanzania hususani katika jamii ya watu waliookoka. Hii ni kwa mujibu wa mchango wao katika kumtangaza Kristo hapa nchini. Kuanzia Tarehe 21/09/2011 mpaka tarehe 25/09/2011 kuanzia saa 09 jioni -12:30 jioni.

 Askofu Emmanuel Lazaro mwenye makazi yake mjini Moshi atakua akifanya semina ya “UREJESHO” katika kanisa la Living water centre lililopo Kawe makuti jijini Dar es salaam. Kanisa hilo linaongozwa na Mtume Onesmo Ndegi pamoja na Mkewe Mama Lilian Ndegi.
Semina hii ya aina yake ambayo siyo ya kukosa,hii ni  kwa kuwa ni mara chahce sana kumkuta Mzee Lazaro akifanya Semina nje ya kanisa lake la TAG ambalo yeye ni mmoja kati ya waasisi wa kanisa hilo nchini.Hii ni moja kati ya ishara ya umoja wa KIROHO katika Mwili wa Kristo hapa nchini.


Kupitia hatua hii ya Mtumishi Ndegi na Askofu Lazaro tunajifunza kuwa japokuwa kati ya dhehebu moja na lingine tunaweza kuwa na tofauti za kimapokeo,Wito,au Tafsiri ya  Neno(Doctrines) lakini tunaweza kuviweka hivyo kando na tukamwabudu Mungu kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...