Monday, September 12, 2011

Lakini Namna Hii Haitoki Ila Kwa Kufunga na Kuomba.



Mathayo 17:12 “lakini namna hii haitoki, ila kwa kusali na kufunga”.

Mpenzi msomaji naamini kwa sehemu huenda unaijua vizuri habari ya Mathayo 17:14-21 “Habari hii inahusu kijana mmoja aliyekuwa na pepo wa kifafa, wanafunzi wa Yesu wakamwombea wasiweze kumponya. Yesu alipokuja toka mlimani akamponya yule kijana. Baadae walipokuwa faragha wanafunzi walitaka kujua kwa nini wao walishindwa kumtoa pepo. Yesu aliwapa sababu 2, moja kwa sababu ya upungufu wa imani yao, na pili akawaambia namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga”.

Sasa mwezi huu nataka tutafakari swali hili kwa pamoja, Je, ni wakati gani/au kwa mahitaji gani unatakiwa kusali na kufunga? Hapa Yesu alimaanisha kuna mambo/maombi mengine hayawezi kujibiwa mpaka kwa maombi ya kufunga.. Sasa swali ni wangejuaje kwamba hitaji hili/namna hii inataka kusali na kufunga au kusali bila kufunga.


Nina amini hata msomaji wnagu una mahitaji mengi unayoombea, yapo ya kwako binafsi, familia, kanisa, nchi, kazi, mume, mke, mchumba, biashara, watoto nk.

Hii ina maana kuna baadhi ya maombi yako hayatajibiwa haraka au kabisa hadi uombe na kufunga. Swali ni Je, unajuaje kwamba sasa natakiwa kusali na kufunga au kusali bila kufunga.

Mambo matatu yafuatayo yatakusaidia;

a)         Kutokuona matokeo ya maombi ya bila kufunga.
Hii ina maana huenda kwa muda mrefu umekuwa ukiombea jambo fulani bila kuona matokeo yake. Usibakie kusema kwamba natakiwa kuwa mvumilivu. Huenda hiyo ni taarifa kwamba ndugu namna hiyo haitoki ila kwa kusali na kufunga. Hivyo ongeza kufunga kwenye maombi yako, utaona matokeo yake kwa kipindi kifupi.

b)        Uzito na uharaka wa suala unaloombea.
Uzito wa jambo unaloombea ni kwa mtu binafsi (too personal). Jambo ambalo kwako ni zito/mzigo kwa mwingine si zito. Mfano suala la binti anayetafuta mume/mtu anayetafuta kazi uzito wa hili suala hauwezi kulingana kati ya mtu na mtu. Huenda huyu dada ameomba miaka 3 na hajaona mtu akija kumsemesha, kwa mtu huyu tatizo hili ni zito sana. Hatua kama hii inamtaka afunge na kuomba.

Mfano mwingine ni hatari ya kifo kama mazingira yaliyowakuta kina Esta katika utawala wa mfalme Ahusuero, pindi ulipoandaliwa mpango wa kuua wayahudi wote, tunaona walifunga kwa siku tatu, au watu wa mji Ninawi walipoambia na Yona kwamba wasipotubu mji wao pamoja na wao wataangamizwa, nao walifunga. jifunze kwa Esta, Daniel, Yona, Nehemia, Yesu n.k



c)   Kwa uongozi wa Roho mtakatifu.
   Mathayo 4:1 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani… akafunga siku arobaini …………”
Awali ya yote kumbuka Roho mtakatifu ni msaidizi  hata kuomba anatusaidia. Roho mtakatifu ndiye anayeleta au kuweka  mzigo wa kuomba ndani ya mtu. Roho mtakatifu ndiye anayejua habari ya mambo yajayo, kwa sababu hiyo huwa anamsukuma mtu kufanya maombi ya kawaida au ya kufunga tegemeana na hitaji husika na kile kilichopo mbele ya mtu husika. Kwa lugha nyepesi Roho mtakatifu humuongoza mtu katika maombi ya kawaida au ya kufunga pia.

Hivyo basi Roho mtakatifu akikuongoza kufunga wewe usimzimshe au usikwepe maana yeye anajua nini kinaenda kutokea mbele yako na kinahitaji nguvu kiasi gain ya maombi ili uweze kuvuka au ili namna hiyo iweze kutoka.

Ni imani yangu kuwa ujumbe huu mfupi utakusaidia kukujengea nidhamu katka maombi yako kwa ujumla na utakuwa makini na maombi unayoyafanya.

Barikiwa na Yesu kristo.

Mwl Patrick Sanga

2 comments:

  1. Kuna Imani na kuamini(Faith and belief). Imani si tatizo kwa Wakristo na uhitaji Imani kubwa(Yesu anasema imani ndogo kama punje ya haradali yatosha).kUTOKUAMINI NDIO TATIZO,ndio maana Baba wa mtoto alijibu vile....help my unbelief.Na aliposema haiji ila kwa...ambayo haiji ni kuondoa kutokuamini sio kuondoa mapepo kwani kutokuamini ndio chanzo cha maombi kutojibiwa..Ubarikiwe mtu wa Mungu

    ReplyDelete
  2. Hello Everybody,

    Below is a list of the highest ranking FOREX brokers:
    1. Most Recommended Forex Broker
    2. eToro

    Here is a list of money making forex tools:
    1. ForexTrendy - Recommended Odds Software.
    2. EA Builder - Custom Indicators Autotrading.
    3. Fast FX Profit - Secret Forex Strategy.

    Hopefully these lists are helpful to you.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...