Wednesday, October 26, 2011

Beatrice Muhone Azindua album yake ya Tatu


Beatrice Muhone akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi wa album yake ya HUNIONGOZA Jumapili iliyopita.

Mwanamuziki Mahiri wa nyimbo za Injili Afrika mashariki na kati Beatrice Muhone mwenye makazi yake jijini Arusha jumapili iliyopita tarehe 23/10/2011 amezidua album yake ya Tatu aliyoipa jina la HUNIONGOZA. Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo alikuwa Mh Ezekiel Maige ambaye ni Waziri wa maliasili na utalii. Uzinduzi huo uliambatana na changizo la fedha kwa ajili ya kusaidia watoto yatima.

Album hii ya Huniongoza inafuataia baada ya Album zake mbili zilizotangulia ambazo ni INGOJE AHADI pamoja na AMEJIBU AHADI. Katika uzinduzi huo Beatrice Muhone alisindikizwa na Upako Group ambacho ni kikundi cha uimbaji wa nyimbo za injili cha mjini Arusha pamoja na waimbaji maarufu wa injili ambao ni Cosmas Chidumule, Ambwene Mwasongwe pamoja na Ado November.

Hosanna Inc alishuhudia jumapili iliyopita jiji la Arusha likiwa na matukio takribani matatu yanayohusu injili ambapo Tukio la kwanza ni hili la Beatrice Muhone Kuzindua Album yake katika Hotel ya Naura Spring , Wakati Beatrice akizindua Album yake, katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mwanamuziki Mwingine wa injili toka jijini Arusha alikuwa akizindua album yake na Mh Tundu Lissu alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo. 

Tukio lingine lilikuwa ni kuanza kwa semina ya Neno la Mungu inayohudumiwa na Mtumishi Engineer  Tumainieli Mbwambo, semina hiyo inaendelea katika Ukumbi wa Metropole ulioko katikati ya jiji hilo.

Kundi maarufu la kusifu na kuabudu jijini Arusha UPAKO SINGERS lilikuwepo ukumbini kumsindikiza Beatrice

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...