Wednesday, October 26, 2011

Campus Night 11-11-2011 Homa ya Jiji


Jamaa anaitwa Freddy Chavalla nI Gospel Comedian atakuwepo siku hiyo pale Leaders Club
Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo Presha na shauku ya Tamasha la CAMPUS NIGHT inavyozidi kuongezeka. Kwa ambao hawajui Tunammanisha nini, Night Campus ni Usiku Maalumu wa Kusifu na Kuabudu ukiambatana na mafundisho ya Kimungu pamoja na mazungumzo yenye kujenga yakiwalenga zaidi vijana hususani walioko vyuoni. Kadri miaka inavyozidi kwenda mbele ndio hasa Night Campus inavyozidi kuwa gumzo kwa kugusa maisha ya Vijana wengi.

Kwa Mwaka huu wa 2011 Campus Night inasimama chini ya Kauli mbiu(Theme) iitwayo FOCUS baada ya ile ya mwaka jana iliyoitwa HIGHER LIFE. Night Campus ni tukio pekee  linalowaunganisha na kuwaweka pamoja wanafunzi waliookoka kutoka vyuo vyote vya jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani hususani Mikoa wa Morogoro na Pwani kwa utukufu wa Mungu.

Campus Night huandaliwa na Vijana wa Kanisa la Victory Christian Centre lililo chini ya Mch Huruma Nkone  kwa Mwaka huu itahusisha wanamuziki na wasanii kutoka Mataifa mbalimbali yakiwemo Uganda, Kenya , Tanzania ,Burundi, na kutoka bala la Ulaya.Ni matumaini yetu kuwa Mungu atashuka na kuhudumia ROHO za Vijana katika kusanyiko  hilo.


Night Campus 2011
Date: 11/11/2011
Venue: Leaders Club Kinondoni
Time:12:30jioni Mpaka asubuhi
Hakuna Kiingilio


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...