Saturday, October 15, 2011

Jehova Yu Hai Tour Kuitikisa Mwanza

John Lisu akiwa studio ya Alive Fm Radio ya jijini Mwanza
Mwanamuziki wa nyimbo za injili John Lisu pamoja na kundi lake wanatarajia kufanya Tamasha la kusifu na kuabudu katika jiji la Mwanza.Kwa mujibu wa John Lisu Tamasha Hilo lainatarajiwa kufanyika Tarehe 6/Nov/2011  kuanzia saa 9:00 Mchana -12Jion katika ukumbi wa Hotel Mpya ya Golden Crest ulioko mkabala na New Mwanza Hotel.

Hapo awali tamasha hilo ilipangwa kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kabla mabadiliko hayajatokea. Hili litakuwa ni Tamasha la Pili kwa John Lisu kuhudumu katika jiji la Mwanza ambapo tamasha lake la awali lilifanyika takribani miaka Mitatu iliyopita.

John Lisu akiwa na Addo Nzwalla ambaye ni mmoja wa watangazaji wa ALIVE FM

Lisu aliiambia Hosanna Inc kuwa anatarajia kufanya Tamasha Hilo LIVE Pasipo Playback. Akiwa jijini Mwanza kwa maandalizi ya Tamasha Hilo Lisu alifanya Mahojiano(Interview) na  mtangazaji Smith Swai kutoka Redio ya  ALIVE FM na kueleza dhana nzima ya Tamasha hilo. Hosanna Inc itakuarifu mchakato mzima katika kuelekea kwenye  Tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...