Sunday, October 9, 2011

Juliani aibuka Mwanamuziki Bora wa Mwaka nchini KenyaJuliani akiwa ameshika Tuzo mbili za Kisima Music Awards alizokabidhiwa  wakati wa Sherehe za Tuzo Hizo kwa mwaka huu wa 2011
Juliani ni Mwanamuziki mahiri wa Muziki wa Gospel HipHop nchini Kenya.katika Tuzo Kongwe nchini Humo zijulikanazo kama Kisima Music Awards zilizomalizika hivi karibuni. Julliani pamoja na kunyakuwa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Gospel Hip Hop, pia amefanikiwa kunyakuwa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Mwaka nchini humo nafasi iliyokuwa ikiwaniwa kwa karibu na mwanamuziki Kidumu pamoja na Jaguar anayetamba na Hit Song iitwayo Kigeugeu.

Kitendo cha  Mwanamuziki wa Injili kunyakuwa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa mwaka nchini humo na kuwaweka kando magwiji wengi, kimepelekea mwanamuziki Huyo kupata Zawadi ya Shillingi Million Moja ya Kenya ambapo zawadi hii inaaminika ni zawadi kubwa ya kwanza kutolewa katika Tuzo za Muziki nchini humo.

Julliani mwenye umri wa Miaka 25 anatamba nchini humo na nyimbo yake ya Gospel iitwayo “Barua ya Ocampo” inayogusa Medani za siasa za sasa za nchi hiyo. Baada ya kupokea hundi ya pesa hizo Julliani alisema atatumia sehemu ya pesa Hizo katika kuendeleza Project iitwayo “Kama Si Sisi” ambayo amekuwa akifanya nayo kazi. Project Hii lengo lake kubwa ni kuwafundisha vijana namna ya kuondokana na majanga mbalimbali yanayoweza kuwakumba katika umri wa ujana.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...