Thursday, October 27, 2011

Kuelekea Miaka 50 ya Uhuru, Watanzania Waishio Marekani na Canada Kufanya Ibada ya Pamoja Kusherehekea UhuruWatumishi wa MUNGU kutoka Tanzania waishio na kuhudumu Nchini Marekani na Canada pamoja na washirika, mnamo Tarehe 12Nov 2011 wanatarajia kukutana na kuwa na ibada ya Pamoja kwa ajili ya kumtukuza Mungu kwa kutuwezesha Tanzania kufikisha MIAKA 50 toka tumepata UHURU. Ibada hiyo itakayohudumiwa na speakers Sita kutoka Huduma(Ministries) tofauti tofauti za watanzania waishio katika mataifa hayo , inatarajia kufanyika katika kanisa la BETHEL WORLD OUTREACH CHURCH lililoko nchini Marekani.

Hii ni fursa nzuri kwa Watanzania waishio Nje ya nchi kukaa pamoja na kumtukuza Mungu kwa Yale yote aliyotutendea kama watanzania. Mungu Wetu ni wa AJABU NA Fadhili ZAKE kwetu Hazikomi kizazi mpaka kizazi.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...