Thursday, October 13, 2011

New Life Band wamwadhimisha Bwana Jijini MwanzaNew Life Band wakiwa jukwaani na Kushoto ni Kiongozi wa Bendi hiyo Fortunatus Mabondo{ONDO}


Bendi Kongwe ya Muziki wa Injili ya New Life Band yenye makazi yake jijini Arusha, Jumapili iliyopita ilifanya Tamasha la WAZI la Kusifu na kuabudu katika jiji la Mwanza. Tamasha hili lilifanyika katika viwanja vya Furahisha na liliandaliwa na umoja wa makanisa jijini Mwanza. Katika Tamasha hilo Makanisa yapatayo Arobaini na Mbili{42} yaliunda Mwanza Mass Choir iliyokuwa na jumla ya Waimbaji zaidi ya Mia na ishirini{120}.


Sehemu ya Mwanza Mass Choir
Kwa wanaofuatilia matamasha ya Muziki wa Injili jijini Mwanza watakubali kwamba hili ni Tamasha la Kwanza la LIVE lililowahi kufanyika jijini Hapa kwa Mwaka huu na kupata ushirikiano wa kutosha kati ya Praise Team na Hadhira.

Tamasha lingine la LIVE lililokuwa bora jijini Mwanza ni la uzinduzi wa Album ya Ni Asubuhi ya Mwanamama  Miriam L. Mauki lililofanyika   katika uwanja wa CCM Kirumba. Mengi ya Matamasha yanayofanyika jijini Mwanza hususani yanayofanywa na wageni{watumishi kutoka nje ya jiji la Mwanza} hutumia PLAYBACK na sio Live na hivyo kukosa ladha halisi ya Muziki.

Katika tamasha Hili ambapo Mama Diana Mwakasege alihudhuria, kuanzia Mwanzo mpaka Mwisho Hadhira ilikuwa ikienda Sambamba na Ebednego ambaye ni Sololist wa Bendi Hiyo. Bendi nzima ya New Life chini ya Mtumishi Mabondo marufu kama ONDO ilikuwepo jijini Mwanza kwa ajili ya Huduma hiyo, ambapo watumishi hao walikuja na SOUND SYSTEM yao kutoka jijini Arusha.

Inafahamika kuwa uwanja wa Furahisha huwa hauna viti, cha kutia hamasa ni kwamba watu walikuwa wakiimba na kucheza kuanzia Mwanzo wa Tamasha mida ya saa Tisa mchana mpaka tamasha lilipofungwa Rasmi na Askofu Elihuruma Swai wa Kanisa la TAG mnamo saa moja Usiku.

Setting ya Vyombo na stage vilifanyika siku ya Ijumaa na Jumamosi


Hosanna Inc ilipata nafasi ya kuongea na ONDO na kumuuliza

Hosanna Inc: kwa nini mmefanya Tamasha hili jijini mwanza na sio mikoa mingine ya Tanzania Tofauti na Moshi na Arusha ambako mmejikita kwa Muda mrefu?

ONDO: Ulikuwa ni mpango wa Mungu tuje Mwanza na kufanya huduma hii ingawa Mwanzoni tuliona ni gharama sana na unajua kitu chochote cha Kimungu kinaupinzani mkubwa, ila watu wa Mwanza walisimama kwenye Maombi na leo Mungu ametufanikisha.

Maandalizi yakiendelea siku ya Jumamosi

Bro James Kimtuo akipiga kinanda na kuimba siku hiyo

Mass Choir na Hadhira wakimtukuza Mungu

Abiria Chunga mali yako, Soloristi wa New Life Band Mtumishi Abednego akienda sambamba na Mkewe jukwaani
Shangwe kwa Kristo Yesu

Nijaze Roho Mtakatifu, Niwekeeee karibu na weeee Eeeh  Eeeh Nirejesheee Furaha ya wokovu Baba Nafsi yangu Yakutamanii

Askofu Elihuruma Swai akifunga Tamasha mnamo majira ya saa moja usiku

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...