Thursday, October 6, 2011

Sifa zivume DVD Kuzinduliwa rasmi Diamond JubeleeJohn Lissu akiliongoza Kundi la RIVERS OF LIFE siku ya Tamasha la Sifa Zivume katika ukumbi wa Mlimani City

Lile Tamasha la kusifu na kuabudu linalokumbukwa na wengi lililopewa jina la SIFA ZIVUME  lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kugusa mioyo ya wengi. kwa sasa DVD zake zinapatikana na zitazinduliwa Rasmi katika ukumbi wa Diamond Jubelee mnamo tarehe  27-Nov-2011.

Kundi la Rivers of Life kutoka Dar es salaam Pentecost Church(DPC) ambao ndio waimbaji wa DVD hiyo ni moja kati ya makundi yanayoaminika kujipanga vizuri kabla ya kufanya shughuli. Siku kadhaa zilizopita kundi hilo lilizindua AUDIO CD ya Sifa zivume ambapo kwa mujibu wa RIVERS OF LIFE wenyewe ni kwamba kwa yeyote anayehitaji CD Audio hiyo anaweza kupiga simu namba 022-2668821.

John Lissu, Pastor Safari, Minza Nkila na wengineo wengi hawa ni baadhi tu ya waimbaji ambao wanaounda kundi hilo linalopendwa na wengi kwa utumishi wao mbele za Mungu. Na Atukuzwe Mungu awezaye kutenda mambo makubwa nay a ajabu mno kwaq utukufu wake hapa nchini na kote Duniani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...