Wednesday, October 12, 2011

Wakristo wa Dhehebu la Kikoptika waandamana nchini Misri


Wiki iliyopita Wakristo wa madhehebu ya Kikoptiki nchini Misri walishiriki katika mgomo wa kukaa barabarani huku polisi wakisimama katika hali ya ulinzi mbele ya jingo la Televisheni ya Taifa kusini wa mji wa Cairo.

Wakoptiki hao waliitisha mgomo huo wakidai gavana wa jimbo la Aswan Mustafa el Sayed ajiuzulu na Kanisa lijengewe tena katika kitongoji cha Marinap katika jimbo la Aswan nchini humo.

Wakoptiki walijenga tena jengo liliwahi kuwepo kijijini hapo Marinap na kulihamishia Kanisani bila kibali cha mamlaka husika hali ambayo iliwaudhi waislamu waishio kijijini humo ambao walifanya Jaribio la kubomoa jengo hilo. Tukio hilo liliamsha tena uhasama kati ya makundi hayo mawili ya kidini.

Kundi la waislam baada ya kumaliza sala ya ijumaa wiki iliyopita, walienda kanisani hapo na kuanza kubomoa jengo lote, lakini majeshi ya usalama yaliingilia kati hali iliyosababisha sehemu ndogo tu ya ukuta na nguzo mbili za sementi kubomolewa.

Wakoptiki walichukizwa na matamshi ya el-Sayed yaliyodai kwamba idadi ya Wakoptiki ni ndogo sana kiasi cha kuhitaji kujengewa Kanisa na kwa kuwa kuna kanisa  kuna lingine umbali wa kilomita mbili hivyo hakuona umuhimu wa kujengwa kwa kanisa mahali hapo kauli ambayo ilipelekea maandamano hayo.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...