Friday, October 28, 2011

WOW Album For 2011 iko Sokoni


Wow album ni mtiririko wa wa Video Album za Injili chini ya Lebo Mahiri duniani iitwayo VERITY. Wow hujumuisha nyimbo toka kwa wanamuziki mbalimbali wa injili Duniani wakubwa kwa wadogo na hatimaye hutengeneza collection Album ambayo ndio hupewa jina la WOW ALBUM.

Kwa mujibu wa official Website ya lebo ya Verity, Wow 2011 inajumuisha wanamuziki kama Donnie Mcclurkin, smokie Norful, Fred Hammond, Shekinah Glory Praise and Woship Team ikiongozwa na Smash aliye-lead humo ndani a hit song inayoitwa “Praise is what I do” na wengine wengi.

Smokie Norful Mmoja kati ya watumishi waliohudhurisha Sauti zao katika Wow Album 2011

Collection Album hii imekuwa Released mapema Mwaka huu lakini kulingana na upatikanaji wake nchini Tanzania ni wachache sana waliofanikiwa kuipata mpaka muda huu. WOW ALBUM zilianza kutoka rasmi mwaka 1998 na hadi kufikia sasa zimeshatoka jumla ya WOW ALBUM zipatazo kumi na mbili. Hapa nchini Msama Promoters wanadesturi ya kuandaa Collection album ambazo wamezipa jina la Halleluya album collection. 
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...