Monday, November 21, 2011

Mch Daniel Kulola Akabidhiwa Digrii ya Falsafa(PHD) ya Heshima


Dr Daniel Kulola Kulia akiwa akisalimiana na Wakufunzi na wageni Rasmi  mara baada ya kukabidhiwa Digrii ya Falsafa ya Udaktari wa Heshima
Mchungaji Daniel Kulola wa kanisa la EAGT Lumala jijini Mwanza Jumamosi iliyopita 19/11/2011 katika kanisa la MITO YA BARAKA jijini Dar es salaam alitunukiwa Udaktari wa Heshima( PHD) kutoka chuo kikuu cha Calfonia cha Nchini Marekani.

Chuo hiki ambacho ni maarufu Duniani kimeamua kufanya hivyo kwa mtumishi Daniel kulola kufuatia mchango wake katika kueneza injili Barani Afrika na Duniani kwa ujumla kwa kupindi cha Miaka 22 ya utumishi wake.

Sambamba na tukio hilo, pia kuliambatana na Mahafali ya kutunukiwa DIPLOMA wanachuo wa chuo cha Biblia cha EAGT TEMEKE ambapo wanachuo 41 walihitimu.
 
Mgeni Rasmi kwa sherehe hiyo alikuwa ni Profesa na Dr. Edward Nasioki ambaye ndiye mkurugenzi wa Mafunzo kwa nchi zote za africa na pia ndiye mwakilishi wa shirika la Haki za Binadamu kutoka umoja wa mataifa anaishi California. Nchini Marekani.
Katika hotuba yake Dr Nasioki alisema Dr. Daniel kulola ndiye mwafrika wa kwanza kupata shahada hii ya PhD bila kutoa malipo yoyote ambapo wengine hutakiwa kulipa $ 6,000  kwa watu wa kawaida na kwa viongozi wa serikali duniani hulipia $ 12,000

Dr Daniel Kulola akifuatilia kwa makini shamlashamla hizo

Hosanna Inc ilimuuliza Dr Daniel Kulola  kwa alikotoka  hadi hapa alipofikia kama mtumishi wa Mungu anaushauri gani kwa Watumishi wengine,na Hivi ndivyo alivyojibu

Dr Kulola: Kama vile mimi nilivyo msubiri Mungu kwa uvumilivu wa muda mrefu miaka 22 tangu Mungu alivyosema na mimi  Mwaka 1990 nikiwa Geita kwa nguvu akisema niachie Mwanza , Akaniambia “utahubiri mwanza, tanzania, africa yote na ulimwenguni kote” na sasa  yametimia. Cha msingi hapa ni kuwa mvumilivu na kufanya kazi kwa nguvu bila kukata tamaa, lakini pia kujishusha wengi wa watumishi hawapendi kuwa watu wa kawaida,wana majivuno, kiburi na mengine, pia kuitunza imani iliyo safi. Nimekataa kujiingiza katika imani za mpito. Katika kutenda haya watu  wengi duniani wanafuatilia kwa karibu ikiwa ni pamoja na vyuo.

Watumishi tuwe na hali ya kumsubiri Mungu kuliko tuharakishe na kutaka matakwa yetu wenyewe lakini pia kukubali kuonywa na kukemewa na wale waliotutangulia, jambo hili mimi limenisaidia.

Huduma yangu imesambaa kote sasa Tanzania, Africa, Ulaya na america pia mwakani naendelea Namibia, Botswana, South africa, Uingereza, Scotland, Denmark, Sweden, Norway, America. Nasema hivi kwani tayari mialiko imekwisha kaa sawa na ni wakati wa kutangaza neno la Mungu. alisema Dr. Daniel Moses Kulola.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...