Thursday, November 10, 2011

Mchungaji Daniel Kulola kutunukiwa Udaktari(Phd) wa Heshima


Mchungaji Daniel Kulola

Mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala jijini Mwanza Mchungaji Daniel Kulola, mnamo tarehe 19/Nov/2011 katika kanisa la EAGT Mito ya Barajka la jijini Dar es salaam atakuwa akitunukiwa Digrii ya UZAMIVU=PhD (udaktari wa Heshima) kutoka chuo kikuu cha California state University cha NCHINI Marekani.

Chuo hiki ambacho ni maarufu Duniani kimeazimia kufanya hivyo kwa mtumishi Daniel kulola kufuatia mchango wake katika kueneza injili Barani Afrika na Duniani kwa ujumla kwa kupindi cha Miaka 22 ya utumishi wake.

Katika hali ilioonyesha kuthamini Utumishi wa Baba yake Daniel Kulola yaani Mzee Moses Kulola, chuo hicho kimeamua pia kitamtunuku Udaktari wa Heshima Askofu Moses Kulola kwa utumishi wake wa Miaka 65 katika Taifa la Tanzania na nje ya nchi.

Wakati  siku hiyo ya Tarehe 19/111/2011 wote kwa pamoja Baba na Mwana watakuwa wakitunukiwa Udaktari wa Heshima kwa utumishi wao Mbele za Mungu. kwa Mch Daniel Kulola itakuwa ni mara ya kwanza kutunukiwa, kwa upande wa Askofu kulola hii ni mara ya Pili kutunukiwa heshima Hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...