Sunday, November 27, 2011

Testimony: Siri ya Marehemu Dr Remmy Ongala Kufuga Nywele


Dr Remmy Ongala akijisomea Neno la Mungu

Ramadhani Mtolo ndio jina halisi la Marehemu Dr Remmy Ongala, alikuwa Mwanamuziki wa nyimbo za Kidunia(Circular Music) na baadaye  alipata Neema ya Kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wa Maisha Yake Miaka Michache kabla ya Kifo chake.

Dr Remmy Ongala alizaliwa nchini Congo Kinshasa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu, Mama yake mzazi alikuwa ameshajaliwa kujifungua watoto wawili ambapo kwa bahati mbaya wote walifariki. 

Watoto hawa hawakuwa Mapacha na aliwazaa katika vipindi viwili tofauti na kila mmoja alifariki kwa wakati tofauti. Mama huyo alipopata ujauzito wa tatu akaona inawezekana kabisa mtoto huyo akafariki kama walivyofariki wengine wawili waliotangulia.

Baada ya kujiuliza Maswali kwa muda mrefu pasipo majibu ndipo siku ya siku alijifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Ramadhani ambaye ndiye Remmy.Kwa kuwa mamaye  Remmy hakutaka kumpoteza  mwanaye, akaamua kwenda kwa mganga wa Kienyeji ili kupata Kinga itakayoyasalimisha maisha ya Mwanae.

Alipofika kwa Mganga wa Kienyeji, mganga alimwambia ili mtoto wake asifariki inabidi mtoto huyo(Remmy) asinyolewe nywele  Maishani mwake ushauri ambao mamaye aliupokea na kuufanyia kazi. Remmy alizaliwa akiwa tayari na meno mawili ya mbele kitu ambacho kilichukuliwa kama ishara ya baadaye kuja kuwa mganga wa kienyeji ingawa utabiri huo haukutimia. Hivyo toka akiwa mtoto mdogo Dr Remmy hakukatwa Nywele na hata alipokuwa mkubwa na kulijua hilo halikumsumbua sana kwa kuwa alikuwa keshazoea kuishi kwa staili hiyo.

Remmy aliingia nchini mwaka 1978 na katika kipindi chote hicho alikuwa akifanya kazi kama Mwanamuziki wa Circular Music. Alifariki mwaka 2010 jijini Dar es salaam, miaka michache kabla hajafariki Dr Remmy alimpokea YESU kama Bwana na Mwokozi wa MAISHA Yake. Baada ya kuokoka Dr Remmy alikuwa akisali katika kanisa la Glory of Christ  lililoko Ubungo jijini Dar es salaam. Watumishi kanisani hapo walimshauri anyoe Nywele kama moja ya Hatua za Kuvunja maagano yaliyowekwa hapo awali kitendo ambacho Dr Remmy alikubali na kunyoa rasta hizo. 

Baada ya kuokoka Remmy alisema katika maisha yake alikuwa akiudharau wokovu na hakuwahi hata kufikiri kuwa ipo siku atakuja kuokoka au kukata nywele. Biblia inasema  “All things works together for Good”, Safari ndefu ya maisha ya Dr Remmy ikaishia Madhabahuni. Album yake ya Injili aliyoipa jina la “Kwa Yesu kuna Furaha” iligusa mioyo ya watu wengi kwa kuwa ilibeba ushuhuda wa maisha yake.Remmy alibatizwa kanisani hapo kisha akaanza kumtumikia Mungu kama muimbaji wa nyimbo za injili mpaka mwisho wa uhai wake. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...