Wednesday, December 28, 2011

Mch Goodluck Kyara zao lingine la TAFES – SAUT kuwekwa wakfu jumapili Ijayo

Mch Goodluck Kyara jumapili ijayo ya Tarehe 01-01-2012 katika kanisa la Mwanza International Community Church{MICC} atakuwa akiwekwa wakfu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya Uchungaji. Ibada hiyo ya Ordination itaongozwa na Mch Zakayo Nzogele  ambaye ni Senior Pastor wa Micc.
Mch Kyara ni Kiongozi na mmbeba maono wa huduma ya NEW VINE INTERNATIONAL MINISTRY  ambayo ndani yake kuna New Vine Christiana Centre Itakayokuwa ikifanya ibada zake Nyegezi jijini MWANZA.

Pastor Goodluck Kyara
Kwa ambao wanamfahamu Pastor Goodluck amekuwa na maono hayo miaka Mingi iliyopita na mwezi wa Tano mwaka huu wa 2011, akiwa Mwaka wa Tatu katika chuo Kikuu cha Mt Augustino( Saut) aliiambia Hosanna Inc kuwa  mwakani naanza kazi Rasmi ya kumtumikia Mungu  kama full time pastor na kwa msaada wa Mungu maneno hayo yanaenda kutimia. Mch Kyara alifunga ndoa mwaka 2010 na ni baba wa mtoto mmoja aitwaye Charity ambaye kwa sasa anamiezi kadhaa,Pastor Goodluck amegraduate Saut  mwaka huu wa 2011.

Kabla ya kuwa Mchungaji Pastor Goodluck amekuwa katibu wa huduma ya CRMI ambayo huuendesha Semina mbalimbali jijini Mwanza na pia kwa muda mrefu sasa amekuwa ni mmoja wa wanakamati wanaoandaa mikutano ya Mwl Christopher Mwakasege jijini Mwanza. Pastor Goodluck akiwa SAUT alikuwa katibu wa Tafes{Umoja wa wanachuo waliookoka} na pia alikuwa Mwenyekiti wa Tafes mkoa wa Mwanza 2010-2011.
Ndani ya Tafes Saut Pastor Goodluck Kyara amekuwa Mtumishi wa tatu kuingia katika huduma kama full me Pastor. Watumishi wengine ambao wako kazini ni pamoja na
1.    Mch Emmanuel Fabrick ambaye ni Senior Pastor wa Zablon Ministry [Mwanza}
2.    Mch Amon Mwakalinga yeye ni Assistant Pastor  TAG Luchelele
Tofauti na hao Mch David Fumbuka Mwakyusa(Former chairperson  of Tafes Saut 2009-2011) yeye bado ni mwanafunzi wa Mwaka wa nne katika kitivo  cha Sheria chuoni hapo na aliingia chuoni akiwa tayari ni full Time pastor jijini Mbeya.

Pastor Goodluck kyara akiwa na mkewe siku ya Graduation yake Dec 2011

Kuingia kwa Pastor Goodluck rasmi katika utumishi ni changamoto kubwa kwa Vijana ambao wako vyuoni, wamemaliza, au wako maofisini ambao Mungu amesema nao wamtumikie ila wanahofia kuingia katika huduma. GOD who started his work in him(Pastor Goodluck) will come to accomplish it.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...