Friday, December 9, 2011

Uche Kuongoza Sifa Jijini Nairobi 12-Dec-2011


Uche Agu 
Mwanamuziki Wa Injili Raia wa Naigeria aishiye nchini Afrika ya Kusini aitwaye Uche Agu Maarufu kama Uche Double Double, Tarehe 12 Dec 2011 anatarajia kuongoza sifa na kuabudu katika jiji la Nairobi.Tamasha hilo limeandaliwa na kanisa la Jesus Cerabration Centre la nchini Humo.

Ujio wa Uche nchini humo umetokama na mualiko wa Kanisa hilo wing ya Mombasa linaloongozwa na Rev Dr Wilfred Rai, kwa mujibu wa Pastor Lai ujio wa Uche ni sehemu ya Kumalizia semina iliyoanza 4Dec Mpaka 11Dec ambapo Tarehe 12 Dec  uche atapanda jukwaani. Semina hii ilikuwa maalumu kwa ajili ya Wachungaji na Viongozi wa makanisa.

Concert hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Nairobi Sinema kuanzia saa 9:00 Mchana,Kiingilio ni Ksh 200. Hii itakuwa ni mara ya Pili kwa Uche kupanda jukwaani chini Kenya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...