Tuesday, December 20, 2011

Video Making ya “Tutafika” ya Neema Lyimo


Neema Archbald Lymo ni Mtumishi wa Mungu anayemtumikia Mungu kwa njia ya Uimbaji, Neema alianza rasmi kuimba nyimbo za injili mwaka 2000 na kwa sasa anasali Living Water Kawe Makuti chini ya Apostle Onesmo Ndegi.Kuanzia mwezi wa Saba mpaka wa Tisa mwaka huu wa 2011 Neema amekuwa aki-shoot Video ya album yake ya Kwanza iitwayo TUTAFIKA.

Album hii ya Tutafika ina Jumla ya Nyimbo Nane ambazo ni

TUTAFIKA
FLY HIGH
NIGUSWE NAWE
NYOTA YA ASUBUHI
MAISHA
NEEMA YAKO YATOSHA
LIPO JINA
NIMEKUJA KWAKO

Neema ameiambia Hosanna Inc kuwa Video album hii imefanywa na Kampuni iitwayo Holly Pictures iliyoko Sinza Palestina wakati Audio imefanywa katika studio mbili tofauti Pro-Arts Production pamoja na Zoom Records zote za jijini Dar es salaam. Mpaka sasa Neema ameachia video kadhaa kwa ajili ya kuitambulisha album.  Album hii inatarajiwa kusambazwa na kampuni ya Msama Promotion na itakuwa sokoni Jan 2011.

Neema Lyimo akiwa mbele ya Camera

Harakati Zikiendelea

Dancers wakimtukuza Mungu

Cameraman wa  Holly Pictures ikihahikisha picha nzuri zinapatikana

Shughuli ikiendelea


Crew ya Holly Pictures ikiwajibika

All things works together for Good

Hahaa Close-up Shoot taken

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...