Friday, December 30, 2011

KWA NINI MUNGU ANATAKA TUENENDE KWA ROHO? 1





Ukisoma katika warumi 8:14 Biblia inasema “kwa kuwa wote wanaoongozwa  na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” na pia Paulo kwa wagalatia anasema” Basi nasema Enendeni kwa Roho,wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili Wagalatia  5:16.


Hapa tunaona jinsi Paulo anavyosisitiza kwa makanisa ya Rumi na korinto kuhusu suala zima la kuongozwa  na Roho  Mtakatifu. Anawaambia warumi kwa  kuwa wote wanaongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana  wa Mungu maana yake haijalishi  ana umri gani, ni wa dhehebu gani, jinsia gani maadamu anaongozwa  na Roho wa Mungu huyo ni mwana wa Mungu na bado anawaagiza wagalatia akisema Basi nasema  enendeni   kwa Roho………….. anaposema enendeni maana  yake  mkiongozwa  na Roho, au mkimfuata  Roho katika yale anayowaagiza. 



Maneno haya yanaonyesha  zipo sababu za msingi  kwa nini tunatakiwa kuongozwa  na Roho  sasa hapa sizungumzii kazi za Roho mtakatifu najua zipo kazi nyingi anazozifanya Roho Mtakatifu lakini mimi nazumgumzia sababu za kuongozwa  na Roho Mtakatifu, ambaye ndio agano jipya la Mungu kwetu (Yeremia 31:31) katika hiyo Yeremia Neno linasema “Angalia siku zinakuja asema Bwana nitakapofanya  agano jipya na nyumba ya Israel. Sasa ukiendelea kusoma mistari inayofuata utaona anazungumzia habari za kutia sheria yake katika mioyo ya watu.

Sasa hili ndilo agano jipya la Mungu pamoja na wanadamu. Sasa usipojua kwa nini unatakiwa kuongozwa na Roho na siyo akili zako, au mazoea, au taratibu za kwako n.k. hautajua umuhimu wa kuongozwa na Roho Mtakatifu na pili hautaona sababu za kuongoza na Roho Mtakatifu. Sasa  lengo la ujumbe huu ni kukufundisha sababu za msingi  za kwa nini unatakiwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na siyo akili  zako au mawazo yako. Sasa baada ya utangulizi huo mfupi na tuangalie sababu hizo za msingi.

Moja,

Ili tusizitimize tamaa za mwili wagalatia 5:16

“Basi nasema enendeni kwa Roho , wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.Tunatakiwa tuenende kwa Roho ili tusizitimize tamaa za mwili. Siku zote mwili na Roho ni maadui nia ya mwili ni mauti na nia ya Roho ni uzima na amani (Warumi  8:7). Maana  yake siku zote mwili utakuongoza kufanya mambo ambayo mwisho wake ni mauti ya kiroho na  hata kimwili pia.

Utakuongoza katika  tamaa zake, sasa usipoongozwa na Roho huwezi  kujizuia kutekeleza tamaa za mwili na kwa sababu hiyo wewe si mwana wa Mungu   na mtu wa namna  hii hataingia mbinguni kamwe.  Katika 1Wakorinto 6:9-10 anasema “Au  hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme  wa Mungu? Msidanyanyike, waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala  waabudu  sanamu, wala wazinzi, wala  wafiraji, wala walawiti, wala walevi, wala watamanio, wala walevi wala   watukanaji, wala wanyang’anyi.Sasa utakapoongozwa na Roho Mtakatifu utaratibu wake utakuacha huru mbali  na hayo mambo ya mwili au nia ya mwili na utakuongoza katika uzima  na amani  na kulitenda tunda la Roho ambalo  ni upendo, furaha, amani, uvumilivu utu wema  , fadhii, uaminifu, upole na kiasi “Wagalatia 5:22-23”.

 Mbili,

Ili tupate kuyaelewa mafumbo ya Mungu  na kuyafasiri mambo ya Rohoni kwa maneno ya Rohoni.

1Wakorinto 2:10 inasema “ Lakini  Mungu  ametufunulia  sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote hasa mafumbo ya Mungu” na ule mstari wa 13 unasema “ Nayo twayanena , si kwa maneno yanayofundishwa  kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa  na Roho, tukiyafasiri mambo ya Rohoni  kwa maneno  ya Rohoni. Hapa najua walio  wachungaji, walimu  wa neno la Mungu au viongozi wa vikundi mbalimbali vya kiroho watanielewa zaidi.


sikiliza Roho Mtakatifu ndiye mwenye uwezo wa kuchunguza kilichopo kwenye ufahamu wa Mungu kuhusu wewe, ndoa yako, kanisa lako, biashara yako, masomo yako, nchi  yako n.k. sasa akishachunguza ndiyo anakujulisha maana wewe ulikuwa hujui. Pia Roho Mtakatifu ndiye  anayekusaidia kuyanena, kuyafundisha au kuyafafanua maneno ya Mungu kwa  watu wake,  anaposema kuyafasiri  maana yake kuyafundisha mambo ya Rohoni kwa jinsi / namna ya Rohoni.

 Hivyo kama  wewe ni kiongozi au mwalimu wa neno  la  Mungu, ukiongozwa na Roho, yeye atakuongoza / atakusaidia kuwafundisha hao watu neno la Mungu kwa jinsi  ya Rohoni yaani kwa mfumo wa Rohoni kulingana na watu ulio nao, maana yeye ndio mtunzi wa hilo Neno,soma mwenyewe 2Petro 2:21” maana  unabii haukuletwa popote kwa mapenzi  ya mwanadamu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


 Na; Patrick Sanga.

Thursday, December 29, 2011

Mtumishi Lusekelo asema mvua itakayonyesha Leo jijini Dar es salaam haitokuwa na madhara.


Mtumishi Anthony Lusekelo


 Asema Mvua ni Baraka na sio mpango wa Mungu Mvua kunyesha na kuua watu.
Asema Watu wamezoea kusoma tu kwenye Biblia Kuwa Mungu alisimamisha Jua, Mungu alitawanya Bahari sasa nasema hiyo mvua haitonyesha.
A sema endapo Mvua zitanyesha leo jijni Dar es salaam na kisha zikaleta madhara basi atajiuzulu uchungaji

Mtumishi Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana usiku kupitia Kituo cha Television cha Chanel Ten  aliwaambia watanzania hususani waishio Dar es salaam kwamba pamoja na Idara ya hali ya hewa nchini kutangaza kuwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo alhamisi 29-31/12/2011 mvua kubwa zitanyesha jijini  Dar es salaam na sehemu zingine za nchi, mvua hizo hazitareta madhara kama ilivyotokea siku chache zilizopita ambapo mvua hizo zilisababisha mafuriko kwa wakazi wa mabodeni jijini Dar es salaam na kupelekea vifo vya watu zaidi ya Arobaini.

Mtumishi Lusekelo alisema” Mvua ni Baraka na sio mpango wa Mungu Mvua kunyesha na kuua watu, Mimi Anthony Lusekelo nina nguvu kuliko hiyo mvua  na kama itanyesha Haitokuwana na madhara”. Aliendelea kusema kuwa “Mimi kama mtumishi wa Mungu hiyo mvua haitonyesha na watu wamezoea kusoma tu kwenye Biblia Kuwa Mungu alisimamisha Jua, Mungu alitawanya Bahari sasa nasema hiyo mvua haitonyesha, naweza leta mvua naweza sitisha mvua nmeshakaa kwenye magoti”.

Katika hali ya kuonyesha msisitizo juu ya kauli yake Mchungaji Lusekelo alienda mbali zaidi na kusema endapo Mvua zitanyesha leo jijni Dar es salaam na kisha zikaleta madhara basi atajiuzulu uchungaji. Akaendelea kusema kuwa na wale wote ambao huwa hawaamini mambo ya Mungu na waamini baada ya mvua kutonyesha siku ya leo. Mtumishi Lusekelo alisema wakati mvua ziliponyesha na kuleta madhara yeye hakuwepo jijini Dar es salaam.

Mtumishi Lusekelo awali kabla hajaanza kuwaambia mamilioni ya watanzania juu ya AGANO lake hilo na MUNGU, alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu maoni yake  katika miaka Hamsini ya Uhuru. Alisema Pamoja na changamoto tulizonazo kama watanzania, bado kuna Mengi ya Kujivunia kwa hapa Mungu alipotufikisha.

Wednesday, December 28, 2011

Mch Goodluck Kyara zao lingine la TAFES – SAUT kuwekwa wakfu jumapili Ijayo

Mch Goodluck Kyara jumapili ijayo ya Tarehe 01-01-2012 katika kanisa la Mwanza International Community Church{MICC} atakuwa akiwekwa wakfu kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya Uchungaji. Ibada hiyo ya Ordination itaongozwa na Mch Zakayo Nzogele  ambaye ni Senior Pastor wa Micc.
Mch Kyara ni Kiongozi na mmbeba maono wa huduma ya NEW VINE INTERNATIONAL MINISTRY  ambayo ndani yake kuna New Vine Christiana Centre Itakayokuwa ikifanya ibada zake Nyegezi jijini MWANZA.

Pastor Goodluck Kyara
Kwa ambao wanamfahamu Pastor Goodluck amekuwa na maono hayo miaka Mingi iliyopita na mwezi wa Tano mwaka huu wa 2011, akiwa Mwaka wa Tatu katika chuo Kikuu cha Mt Augustino( Saut) aliiambia Hosanna Inc kuwa  mwakani naanza kazi Rasmi ya kumtumikia Mungu  kama full time pastor na kwa msaada wa Mungu maneno hayo yanaenda kutimia. Mch Kyara alifunga ndoa mwaka 2010 na ni baba wa mtoto mmoja aitwaye Charity ambaye kwa sasa anamiezi kadhaa,Pastor Goodluck amegraduate Saut  mwaka huu wa 2011.

Kabla ya kuwa Mchungaji Pastor Goodluck amekuwa katibu wa huduma ya CRMI ambayo huuendesha Semina mbalimbali jijini Mwanza na pia kwa muda mrefu sasa amekuwa ni mmoja wa wanakamati wanaoandaa mikutano ya Mwl Christopher Mwakasege jijini Mwanza. Pastor Goodluck akiwa SAUT alikuwa katibu wa Tafes{Umoja wa wanachuo waliookoka} na pia alikuwa Mwenyekiti wa Tafes mkoa wa Mwanza 2010-2011.
Ndani ya Tafes Saut Pastor Goodluck Kyara amekuwa Mtumishi wa tatu kuingia katika huduma kama full me Pastor. Watumishi wengine ambao wako kazini ni pamoja na
1.    Mch Emmanuel Fabrick ambaye ni Senior Pastor wa Zablon Ministry [Mwanza}
2.    Mch Amon Mwakalinga yeye ni Assistant Pastor  TAG Luchelele
Tofauti na hao Mch David Fumbuka Mwakyusa(Former chairperson  of Tafes Saut 2009-2011) yeye bado ni mwanafunzi wa Mwaka wa nne katika kitivo  cha Sheria chuoni hapo na aliingia chuoni akiwa tayari ni full Time pastor jijini Mbeya.

Pastor Goodluck kyara akiwa na mkewe siku ya Graduation yake Dec 2011

Kuingia kwa Pastor Goodluck rasmi katika utumishi ni changamoto kubwa kwa Vijana ambao wako vyuoni, wamemaliza, au wako maofisini ambao Mungu amesema nao wamtumikie ila wanahofia kuingia katika huduma. GOD who started his work in him(Pastor Goodluck) will come to accomplish it.

Upendo Kilahiro - Hakuna Usiloweza


Mkesha kabambe wa kuukaribisha Mwaka 2012



The Purposes of God for Christians in Business

It was interesting to hear Mark Bilton speak about being "Called to Business" last night. Mark is the CEO of the Hagameyer multinational which controls several prominent brands, and turns over 300 million a year. He is also a dedicated Christian who sees his work as a big part of his ministry for God. Here are some of the key points from his message:

* Something about WORK itself honors God.
* God ordained work from before the Fall of Man - Adam had to keep the garden.
* The four main reasons God has called people into business are: 1. to Serve God in that function 2. To Co-create something with God. 3. For Provision of needs so we can be in a place where we can be generous. 4. To witness to others.


* We should always have the ability to give something away.
* Signs that we are caught up in covetousness are
 1. We are working TOO MUCH.
 2. We have taken on TOO MUCH DEBT.

* We are called to be generous with time, encouragement and money.
* Even the Good Samaritan needed to have a couple of coins and a donkey so he could be useful in helping.
* Money is a tool. It is not evil. The love of money is evil.
* The profit motive is not wrong, if it is balanced by generosity and bridled by ethical practices in the pursuit of it.
* Companies create wealth, provision and profit.
* Witnessing through your business comes as you show care and concern for fellow employees, as you succeed with God's help. These things create a testimony for God's glory.

* Colossians 3:23,24  says: And whatever you do, do it heartily, as to the Lord and not to men, knowing that from the Lord you will receive the reward of the inheritance; for you serve the Lord Christ.  Our jobs are therefore a form of service to Jesus Christ.

* God says, "In all your ways acknowledge Him, and He will direct your paths" (Proverbs 3:6). We cannot leave God out of our business life. God wants to be involved.

* God's Word reveals that God is even interested in the quality of work and the attitude of a slave.
* God worked for 6 days in Creation before resting.
* It wasn't "work" that was cursed, but the ground, in Genesis 3.
* "Brother Lawrence" talked about the power of being conscious of the presence of God even in daily kitchen chores.
* We bring the Holy Spirit into our business environments and can change the atmosphere of a situation.

* We can bring reconciliation.
* In business we bring VALUE, we bring ORDER, we create JOBS, WEALTH
* The role of economics has risen in world affairs, as the role of politics has somewhat declined.

* God's work has to be done God's way to get God kind of results. Do it God's way 100%.
There was another part of Mark's message, on "Business Transformation" that I will make the subject of another post, God willing.

Tuesday, December 27, 2011

MAASKOFU nchini wametumia ibada za  Sikukuu ya Krismasi kuwataka viongozi wa umma nchini kuacha ubinafsi, tamaa na kujilimbikizia mali kwa sababu tabia hizo zinaweza kuliingiza taifa katika machafuko.

Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akisalimia watoto nje ya lango kuu la Kanisa la Azania Front baada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismasi jijini Dar es Salaam. (Picha na Mohamed Mambo)

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Tabora, Mhashamu Paul Ruzoka, amesema tabia hizo zimekuwa ikiwafanya wananchi wakate tamaa, kwa sababu inawasababisha viongozi wenye tamaa kushindwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na hivyo kugeuka kama maadui wao kwani wanashindwa kutenda haki.

Akihubiri katika Ibada ya Krismasi Kitaifa jana katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Mtoto wa Yesu mjini Tabora, Askofu Ruzoka, pia aliwataka viongozi kuhakikisha kuwa utekelezwaji wa sera ya Kilimo Kwanza nchini, haiathiri wananchi na kuwaacha bila ya kuwa na ardhi.

Akizungumzia athari za kutokuwepo kwa Azimio la Arusha, alisema ni pamoja na kuwepo kwa mbio za utajiri baina ya viongozi, kutofuatwa kwa maadili ya uongozi, kutokuwa na miiko, kuongezeka kwa posho katika vikao vingi na kuibuka kwa mrabaha katika kazi mbalimbali za kiserikali na kukithiri kwa tamaa.

Naye Mchungaji Mwaipopo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kanisa Kuu, Dodoma Mjini, amewataka wabunge kuacha ubinafsi wa kujilimbikizia posho kwani hali ngumu ipo kwa kila Mtanzania.

Alisema anashukuru viongozi kutambua maisha ya Dodoma yako juu kiasi kwamba hawawezi kuishi kwa posho ya Sh 70,000 kwa siku.

Alisema maisha ni magumu Dodoma kwa kila mtu si kwa wabunge tu, iweje kundi hilo dogo lisikilizwe je wananchi wakimbilie wapi?

“Kuna kukata tamaa kila kona, kuna majanga ya kutisha, mafuriko, ajali sasa hivi kifo kimetawala duniani kote.” Alisema Mchungaji Mwaipopo.

Naye Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika, Godfrey Mhogole wa Kanisa la Anglikana, amemlalamikia Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma kwa kufuta matokeo ya watoto waliofaulu darasa la saba mwaka huu.

Alisema iwapo ofisa huyo hataondolewa, yuko tayari kumshitaki kwa kiongozi wa nchi. Alisema kuna haja kwa Ofisa Elimu Mkoa kuangalia kwa kina suala hili kwani halileti picha nzuri katika sura ya elimu nchini.

Alisema katika Shule ya Msingi ya Bishop Stuart DCT iliyopo Msalato mwaka huu walifaulu wanafunzi wanne tu, hali iliyoleta mshtuko kwao.

Alisema kwa miaka mingi shule hiyo imekuwa ikifaulisha sana wanafunzi, lakini anashangaa mwaka huu wanafunzi waliofaulu wamefutiwa matokeo.

Aidha, Askofu Telesphor Mkude wa Jimbo Katoliki la Morogoro, amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha watendaji wa Serikali ‘wachakachuaji’ wanaohusika kwa namna moja ama nyingine kuruhusu wananchi kujenga makazi mabondeni na waliosababisha udanganyifu katika mtihani wa Darasa la Saba.

“Yaliyotokea kwa wenzetu walioathiriwa na mafuriko baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, ni janga kubwa sana na wanahitaji kusaidiwa na Watanzania wote, lakini ninaunga mkono kauli ya Rais Kikwete aliyowaambia waliojenga mabondeni wahame,” alisema Askofu Mkude.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameonya kile alichosema ni baadhi ya watu kuwageuzia na kuwatungia maneno watu wanaojitokeza kupinga dawa za kulevya.

Amesisitiza kuwa dawa za kulevya ni janga la taifa ambalo mapambano dhidi yake hayapaswi kubezwa na mtu yeyote kutokana na namna zinavyoathiri vijana na pia watu wazima.

chanzo: Gazeti la Habari leo

GOSPEL FESTIVAL 2011 YATIKISA MWANZA

Mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Diwani wa Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi Mtumishi wa Mungu Dr. Moses Kulola Cheti kutambua mchango wake katika muziki wa Injili.
Kwaya
Marafiki waalikwa, hapa ilikuwa mwanzo kabisa katika Tamasha hilo kubwa la aina yake lililofanyika leo jioni Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza .
Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tumsifu Rufutu akiwa katika vazi la Musa akiinyoosha fimbo yake kuigiza tendo la kuitenganisha watu mithili ya bahari.
Tumsifu Rufutu aka Musa akiwaongoza wahudhuriaji aka wana wa Israel..
Mara safari ya kuelekea Kaanani kupitia wimbo wake maarufu mwambie Farao ikawadia..
Wageni wetu walio hudhuria tamasha hilo la kwanza lijulikanalo kwa jina la Gospel Festival 2011.
Wageni ni kuimba na kusifu.
Mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi cheti Mtumishi wa Mungu Bishop Charles Sekelwa kwa mchango wake wa kuendeleza muziki wa Injili.
Mtumishi wa mungu Bishop Zenobius Isaya akionyesha cheti alichotunukiwa na Kampuni ya F Plas Intertainment kuthamini mchango wake katika kukuza muziki wa injili.
Mapambano Kwaya kutoka Geita...

Vijana Anglican Nyamanoro Choir wakipata flash ya pamoja.
Wakongwe Aic Makongoro Kwaya nao wakipata flash ambapo hii ni moja kati ya kwaya zilizo tunukiwa cheti maalum kwenye tamasha la Gospel Festival 2011.
Ni fursa ya Moja kati ya Wadhamini Winning Shoping Centre akitangaza huduma zao kwa umati uliohudhuria tamasha hilo pembeni yake amesimama Meneja mipango wa F. Plus Intertainment Albert G. Sengo
Mwimbaji Daniel Safari (R) na (L) wakiwa na mkurugenzi wa F Plus Intertainment Fabian Fanuel (C)
 
Souce:Gsengo

Friday, December 23, 2011

A Christmas Song - Jingle Bells Lyrics




Dashing through the snow
In a one horse open sleigh
O'er the fields we go
Laughing all the way
Bells on bob tails ring
Making spirits bright
What fun it is to laugh and sing
A sleighing song tonight

Oh, jingle bells, jingle bells
Jingle all the way
Oh, what fun it is to ride
In a one horse open sleigh
Jingle bells, jingle bells
Jingle all the way
Oh, what fun it is to ride
In a one horse open sleigh

A day or two ago
I thought I'd take a ride
And soon Miss Fanny Bright
Was seated by my side
The horse was lean and lank
Misfortune seemed his lot
We got into a drifted bank
And then we got upsot

Oh, jingle bells, jingle bells
Jingle all the way
Oh, what fun it is to ride
In a one horse open sleigh
Jingle bells, jingle bells
Jingle all the way
Oh, what fun it is to ride
In a one horse open sleigh yeah

Jingle bells, jingle bells
Jingle all the way
Oh, what fun it is to ride
In a one horse open sleigh
Jingle bells, jingle bells
Jingle all the way
Oh, what fun it is to ride
In a one horse open sleigh
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...