Monday, March 19, 2012

Madhabahu ya Kanisa la Living Water Kawe yatumika kwa ajili ya kuigizia Filamu ya Kikristo



Jumapili ya jana tarehe 18/03/2012 kwenye mida ya saa tatu usiku Television ya East Afrika(EATV) maarufu kama Chanel 5, ilikuwa ikionyesha Filamu yenye maudhui ya Kikristo iitwayo Pastor Myamba Temptation iliyochezwa na  na Macelebrities wawili wa kitanzania ambao ni Emmanuel Myamba(Pastor Myamba) aliyecheza kama Mchungaji na  mwanadada Aunt Ezekiel ameigiza kama Mke wa Myamba.

Wakati Filamu hiyo ikiendelea kurushwa na kituo hicho, Ghafla nilipata simu kutoka kwa wadau wakinitaka niangalie filamu hiyo ilhali tayari nlikuwa naaangalia, na nlipowauliza vipi kwani mtumishi kila mmoja alionekana kushangaa au ku-doubt kwa kitendo cha Madhabahu ambayo imekuwa ikiwafungua wengi, leo watu kuitumia kuchezea mchezo wa kuigiza.kwa utafiti wa haraka haraka Kuna ambao wanahisi si sahihi kwa kuwa ni kuishushia hadhi au kutoiheshimu  Madhabahu,na wengine wanaangalia Motive ya Filamu husika, kama inamafundisho kwa ajili ya Kumtukuza Mungu kwao its oky.


Kwa muda mrefu sasa waigizaji wa Filamu nchini wamekuwa wakitumia mifano ya mazingira halisi ili kupeleka ujumbe,ni mara nyingi badala ya kutumia vituo vya Polisi wamekuwa wakitumia nyumba za kawaida na kuzigeuza vituo vya Polisi,na mifano ya Mahakama badala ya kuigizia katika mahakama halisi.Sasa jana Pastor Myamba alionekana akicheza Filamu hiyo katika Madhabahu ya Kanisa la Living water  Centre(LWC) lililoko Kawe Makuti chini ya  Apostle Onesmo Ndegi.

Mercy Johnson  muigizaji nguli kutoka Nigeria,hapa ilikuwa  siku ya ndoa yake iliyofungiwa katika kanisa la Christ Embassy la nchini Nigeria linaloongozwa na Pastor Chriss Oyakhilome mwaka jana.Ndoa hili ilikuwa ifungwe na Pastor Chriss Mwenyewe kabla hajapata udhuru na kuelekea nchini Uingereza.

Hii sio mara ya kwanza kwa kanisa halisi kutumika kuigizia filamu hapa nchini,utofauti wake unakuja kwa kuwa Kanisa la LWC Kawe Makuti limekuwa ni  kanisa la kwanza kubwa la watu waliookoka kuruhusu madhabahu yao itumike kuigizia Filamu.Good enough ni kwamba Mhusika mkuu wa Filamu hiyo Emmanuel Myamba yeye ameokoka na ni mshirika wa kanisa hilo la LWC.

Katika Filamu hiyo Myamba ameonyesha changamoto wanazokutana nazo watumishi mara baada ya kuitwa kumtumikia Mungu.Humo ndani Myamba alikuwa anaishi na familia yake vizuri huku akifanya kazi kama mwajiriwa wa kampuni.Hivyo alionekana yuko vizuri,baadaye kupitia ndoto Mungu akasema naye njoo unitumikie hali iliyopelekea Myamba kuacha kazi yake na kuanza kuzunguka huku na huko akiihubiri injili ya YESU KRISTO kitendo ambacho kilipingwa vikali na mkewe.

Wakati kitendo cha Apostle Ndegi kuruhusu madhabahu yake itumike kuigizia filamu kikiwashangaza baadhi ya wapendwa,kwa wenzetu sio jambo kubwa ni jambo la kawaida ambapo sio tu watumishi wamekuwa wakiruhusu madhabahu zitumike, wao wenyewe wamekuwa wakiigiza filamu hizo.Kwa uchache tumeshuhudia Bishop Thomas Dexter Jakes akiigiza kwenye Woman Thou art Loosed,amecheza pia kama Mchungaji kwenye Jumping the Bloom filamu iliyotoka mwaka jana mwezi wa tano.

Pichani anaonekana Askofu Thomas Jakes akiongea na Michelle,Jakes  alimtembelea gerezani Michelle baada ya mwanadada huyo kumshoot baba yake wa kambo mbele ya madhabahu ya Askofu Jakes huku Askofu Jakes na kanisa zima likishuhudia.Filamu hii inaitwa Woman Thou art Loosed


4 comments:

  1. Kwanza hiyo filamu ni ya zamani sana Mkuu...
    Pili hebu fuatilia, nadhani ni stori ya Ndegi mwenyewe ile

    ReplyDelete
  2. Yeah its true ni Filamu ya Zamani, kikubwa hapa utagundua kuwa ni mtazamo wa watu kwa kuwa kitendo cha madhabahu kutumika kuigizia Filamu yenye mlengo wa kuujenga ufalme wa Mungu kwa wengi ni kigeni.

    ReplyDelete
  3. Ni vizuri kwa sasa wakristo na wakristu tukabadilisha mtazamo wetu juu ya hili. Ni muhimu sana kwa wacheza filamu nchini wakafikisha ujumbe wao kwa kutumia mazingira halisi kuliko kutumia mazingira artificial.

    ReplyDelete
  4. Mungu atusaidie na tufunguke,mbona viwanja vya mipira vinatumika kwa mambo kibao na wakati mwingine vinatumika pia kwa ajili ya ibada na watu wanaokolewa na wanafunguliwa kwanini wasishangae kwanza kuhusu hilo, Biblia inasema Mungu hakai kwenye jengo Mungu anaishi ndani yako ndio maana ametuita sisi ni hekalu, popote unaweza kumfanyia Mungu ibada na nguvu ya Mungu ikawa kubwa. nafikiri ukiwa mtupi ndani lazima utafute kitu cha kujifunikia,.kama neno linavyosema kwamba watu wangu wanapotea kwa kutokujua maandiko na uweza wa Mungu

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...