Friday, May 11, 2012

Mch Lusekelo asema Mafundisho ya kukana Ukoo ni ya kinyonge na kisaikolojia


Mchungaji Anthony Lusekelo

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa upako amesema kuwa mafundisho yanayofundishwa kuwa watu wakane ukoo au familia kwa kuwa ukoo umebeba roho za mababu na matambiko ni mafundisho ya kishetani na yamejaa hila. Mtumishi huyo akaendelea kusema wengi wa wanaojiita mitume au Nabii huwaambia watu wasipite njia fulani ilihali hawawaonyeshi watu hao njia ipi wapite.Utasikia kama wewe unaitwa Anna, kana jila lako kwa kuwa Anna huwa hawaolewi, je ni kweli Anna wote hawajaolewa?.

Utakuta watu wanakana hadi makaburi ya ukoo wao, twende kwenye Biblia ni wapi watu waliyakana makaburi ya baba zao? Tunayaheshimu makaburi ya babu zetu sio kwa nia ya IBADA, bali kama kumbukumbu ya kule tulikotoka ndio maana wazungu wanaheshimu makaburi ya kwao  hadi kufikia hatua ya kuyalinda.

Akasema leo hii watu wengi wamekuwa wakienda kwa watumishi mbalimbali wakitaka kufanyiwa deliverence kwa kuwa wana mikosi na laana  kisa hawajanikiwi kimaisha, ukweli ni kwamba kati ya watu kumi wanaoenda kwa watumishi ili wafanyiwe deliverence, ni watu wawili tu ndio wanaoweza kuwa na mikosi hiyo au laana wengine nane wote ni wavivu, hawapendi kujibidiisha katika maisha. Wanatumia deriverence kama shortcut  kwa kuwa, kuwekewa mikono na mtumishi ni kitendo cha dakika moja ila kitendo cha kufanya kazi na kuzalisha huchukua muda mrefu.

Akiendelea kuhubiri kanisani kwake , Mch Lusekelo alisema na kwa watumishi, wasiwazuie watu kuhama makanisa , “we wakihama waache wahame,kwa kuwa huwezi Sali kanisa moja miaka kumi, waache waende wakatalii talii kidogo ku-refresh mind kisha watarudi wakiwa wapya”.


4 comments:

  1. Hiyo kusema kwamba eti "hata wazungu wanaheshimu makaburi yao...wanayalinda" sio reference ya kibiblia. Au Pastor Lusekelo hajui kuwa HATA WAZUNGU NAO WALIABUDU NA WANAABUDU MIUNGU NA MASHETANI?

    ReplyDelete
  2. Mchungaji ameeleza vema hakuna sehemu katka biblia inayosema tukane ukoo, kabila hata Yesu mwenyewe ana kitabu kinachoonyesha ukoo aliotokea. Kitu cha msingi watumishi wafundisheni wana wa Mungu kufanya kazi kwa bidii Rev Makenzi

    ReplyDelete
  3. WATU WA MUNGU USIONGELEE JAMBO AMBALO HUNA UFUNUO NALO NA BIBLIA INASEMA USIWE MWEPESI KUJIBU KABLA HUJAELEWA KUFANYA HIVI NI UPUMBAVU ..... KUSEMA KWAMBA JITENGE NA UKOO,HAIMANISHI TUSIWAHESHIMU WA ZAZI AU KUWAMBA TU SIWASILIANE NAOHAPANA NA HAKUNA ANAEFUNDISHA IVO KUJITENGA NA UKOO INAMANISHA KUTO SHIRIKI MATAMBIKO NA MILA POTOVU ZINAZO WAUNGANISHA WATU NA MIZIMU(SHETANI)ILI KUMUISHIA KRISTO,AU NINYI MNA RUHUSIWA KU YAFWATA HAYO MBONA MUNGU ALIPO MWITA GIDIONI ALIMWAMBIA AIVUNJE MADHABAHU YA SANAMU YA BABA YAKE? JE KUFANYA HIVI SI KUJITENGA NA IMANI AU MILA ZA BABA YAKE? JE GIDIONI HAKUENDELEA KUWASILIANA NA NDUGU ZAKE ISIPOKUA IBADA ZAO ZA BAALI????WAKAJA WATU KUMWAMBIA YESU NDUGU ZAKO WAKUSUBIRI NJE, ALISEMAJE? NDUGU ZANGU NI AWA WALIAMINIO JINA LA BWANA ,ALIMANISHA NINI KAMA SI KUONESHA HANA FUNGU NA WASIO AMINI BALI WALE WAAMINIO?? ANGALIA SANA USIWAINGIZE WATU KWENYE IBADA YA SANAMU,HALAFU UKOO WA YESU KUOROZESHWA HAUJAWA NA MAANA YOYOTE KTK MAISHA YA YESU ISIPOKUWA KUELEZEA MTIRIKO WA UNABII WA KUJA KWAKE ULIVYO TEMBEA LAKINI HAKUWA MTUMWA WA MILA ZA UKOO,HIVI UNAELEWAJE MAANA YA KUZALIWA MARA YA PILI??KAMA SIKUFUTA UKURASA WA KWANZA ILI KUZALIWA KATIKA DAMU YA YESU(UKOO WA WATU WA MCHAO MUNGU )MAANA UKOO NI DAMU NDIO MAANA TUMEKOMBOLEWA KWA DAMU YA YESU ,KWAHIYO SISI NI UKOO WA DAMU YA YESU NA SI DAMU KWA JINSI YA ROHO NA SI UKOO WA DAMU YA BABA ZETU... USIWE MTUMWA WA MAWAZO YAKO ,NA KUJITENGENEZEA MADA ZENYE UVUNJIFU WA UMOJA NA USHIRIKIANO KATIKA KRISTO.. KUMBUKA NGOMA IKIZIDI MLIO INELEKEA KUPASUKA,HACHA MANENO YA KUJITOFAUTISHA RAFIKI YANGU ,NAKUPENDA SANA KWAKUSMA UKWELI LAKINI UNAKO KWENDA SIKWENYEWE MNYENYEKEE BWANA AZIDI KUKU INUA MAANA NDIO OMBI LANGU,KUSEMA HILI HALIPO KWENYE MAANDIKO HATA PAULO ALIANDIKA MAMBO MENGINE AMBAYO YESU HAKUYANENA WALA MA NABII KABLA YA NYARAKA ZAKE KUUNGANISHWA NA VITABU VINGINE NALO HILI UTASEMAJE? ROHO,ROHO,ROHO MTAKATIFU BADO YUPO KAZINI HATA SASA, LAKINI USIHACHE KUCHUNGUZA ILI KUUJUA UKWELI...... GIDEON

    ReplyDelete
  4. GIDEONI; marekebisho ya ujumbe hapo juu namaanisha: KWAHIYO SISI NI UKOO WA DAMU YA YESU KWA JINSI YA ROHO NA SI UKOO WA DAMU YA BABA ZETU

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...