Wednesday, November 7, 2012

Namna inavyotishia Kuwa Mkristo nchini Nigeria


Kundi la kiisilamu la Boko Haram nchini Nigeria, na vikosi vya usalama, wote wametuhumiwa na shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International kwa kufanya vitendo vya kukiuka haki za binadamu hasa katika eneo la Kaskazini lenye waisilamu wengi.Boko Haram, ambalo jina lake linamaanisha elimu ya kimagharibi imeharamishwa, kufanya harakati za kuiangusha serikali na kuunda taifa la kiisilamu.


Wanigeria wakifanya maombi

Taarifa zinazohusiana zinasema Siasa Siku ya Jumapili, kanisa lilishambuliwa na kusababisha vifo vya watu wanane mjini Kaduna, mojawapo ya miji ambayo imeathirika kutokana na mzozo unaoendelea kati ya serikali na Boko Haram.Ingawa hawajakiri kufanya mashambulizi hayo, kundi hilo limewajibika wakati lilipofanya mashambulizi Kaskazini na kati kati mwa Nigeria.

Obadiah Diji, kiongozi mmoja wa vijana wa kikristo mjini Kaduna, alisimulia BBC ambavyo maisha yamebadilika mjini humo.“ watu wanaogopa hata kutoka nje usiku au hata kukaa nje tu kunywa pombe au hata kula samaki. Nimeishi mjini Kaduna karibu maisha yangu yote na nimejawa na huzuni sana nikiona ambavyo umegawanyika sana kwa ,misingi ya kidini.

Waisilamu wanaishi ambako idadi yao ni kubwa, wakristo nao vile vile. Kwa hivyo makundi hayo mawili ya watu, yanaishi maisha yao kivyao bila kutangamanaSio kawaida kuwa hivi. Wakati mmoja tulijivunia kwa sababu ya umoja uliokuwa unadhihirika hapa Kaduna na kila mtu alikuwa anakaribishwa hapa.


Ingawa kulikuwa na migawanyiko, wakristo na waisilamu waliishi kwa pamoja. Tulikuwa tunatembeleana . Watoto wetu walisoma katika shule koja , wakijifunza kutoka kwa kila mmoja kuhusu dini na tamaduni zao.

Moja kati ya Mauaji ya Boko Hatamu



Watu hata walioana licha ya dini zao mfano mamangu wa kambo alibadili dini na kuwa muisilamu na kisha akaoa muisilamu. Dadangu pia aliolewa na muisilamu ingawa alisalia kuwa mkristo. Kuna ndoa nyingi kama hizo mjini Kaduna. Haikuwahi kusababisha tatizo lolote. Watu waliheshimiana na kustahimiliana , sio chuki wala ghasia.Mambo yalibadilika mwaka 2000 wakati Kaduna ilishambuliwa kwa mara ya kwanza na mzozo wa kidini ambao unachochewa na makundi yanayotaka sheria za kiisilamu.

Hapo ndipo makundi yaliyohisi kutengwa yalijitokeza. Watu walitoroka makwao kwa sababu ya ghasia. Wakristo walijipata wakiishi katika eneo lao mjini kaduna huku waisilamu nao wakijipata wakiishi maeneo yao.Nimekuwa nikipinga maeneo yaliyotengewa jamii moja na ndio maana bado naishi na mke wake na watoto wetu wanne katika eneo ambalo ni la waisilamu wengi.

Wanawake katika mikutano kadhaa maeneo ya Kaskazini wamepigwa marufuku kubeba vibeti kanisani. Makanisa mengi sasa yana vifaa vya kuwachungua watu wanaoingia kanisani ikiwa wana silaha yoyote au la.Wanawake wanazuiwa kubeba vibeti kwa sababu mshambuliaji anaweza kuingia kanisani akiwahadaa watu kuwa ni muumini kumbe amebeba silaha kwenye kibeti chake.Kwa hivyo maisha yetu ya kidini yameathiriwa sana pamoja na hata maisha ya kijamii.

Sasa tunaishi maisha ya faragha muda wote tukikaa nyumbani. Ni polisi pekee ambao wanapatikana barabarani usiku.Lakini ghasia zimewafanya watu kuwa na imani sana, Wanapata imani hiyo kutoka kwa bibilia ambayo inasema tutapitia mateso kama alivyoteswa Yesu .Ujumbe ambao sisi wakristo tunasambaza ni kwamba waisilamu ni watu wazuri na ni wachache miongoni mwao ambao wanasababisha vurugu, hatapaswi kuvuruga uhusiano kati ya jamii hizo mbili.

Wakati waisilamu waliposherehekea Eid al-Kabir, tuliungana nao katika barabara moja mjini , tulikula pamoja na kusherehekea ili kuimarisha makubaliano ya amani na umoja.Kwa wakati huu, hata mizozo ya kisiasa inageuka na kuwa ya kidini. Siku mbili baadaye, kanisa lilishambuliwa kwa mabomu lakini hilo halitasitisha juhudi zetu za kupatana.

Shule za pamoja

Wakristo na wasilamu husoma hapa na wao ndio tunawategmea kwa mustakabali wetu.Tunatumai watakuwa na kusoma pamoja na kufahamu kuwa tunaweza kuwa watu wa dini mbali mbali lakini bado tunaweza kuishi pamoja.Washambuliaji wa kujitoa mhanga, wamekuwa wakilenga makanisa Kaskazini mwa Nigeria. Ili kupunguza vurugu katika jamii lazima tudurusu mfumo wa siasa zetu. Tunahitaji kuuliza , je Nigeria ilikuwa sawa kuanza kutumia mfumo wa demokrasia ya kimagharibi?

Wanawake waliopoteza jamaa zao kwenye shambulizi la Boko Haram

Hata hatukuwahi kuwa na kiwango hiki cha ghasia wakati wa utawala wa kijeshi.Na hii sio kusema eti lazima tuwakabidhi mamlaka majenerali jeshini.Badala yake, lazima tuangalie,mifumo ya utawala wa kizamamani kabla ya kuja kwa wakoloni.

Tunaweza kujifunza kutoka kwa mifumo hii na kubadili namna ambavyo tunatawaliwa ili ufisadi upungue ,viwango vya umaskini vishuke na kisha ghasia pia ipungue. Mfumo wa kisasa wa maisha umesababisha athari kuliko manufaa. Na leo ni serikali za magharibi pamoja na makampuni ambayo ni chanzo cha vifo vya watu wetu. Makampuni hayo ndio yanatengeza silaha na kuuza kwa mataifa yetu ambayo yanazitumia kwa vita mfano Nigeria na kwingineko.''

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...