Monday, April 30, 2012

Magazeti ya Kikristo kwa ufupi




Kiti namba 666 katika Bunge la Ulaya chazua Balaa

Bunge la ulaya ambalo ndani yake kiti chenye namba 666 kiko wazi

 
Jengo kubwa la mnara wa Ajabu duniani unaosadikika kuwa mnara mwingine baada ya ule wa Baberi linalotumiwa na Bunge la Ulaya lililopo Brussels ubergiji, kwa muda mrefu sasa kiti namba 666 kati ya viti 778 vya wabunge wote wa bunge hilo hakina jina la mtu anayekikalia.Katika viti vyote 778 nina majina majina ya watu wanaovikalia.Mpango wa viti hivyo nadhifu uko nusu duara na viti vinavyokizunguka kti hicho na majina ya wanao vikalia ni kama ifuatavyo

663 Montfort
665Thomas Mauro
666 .............
667 Cappato
668 Turco

Katika mlango mkubwa wa kuingilia katika jengo hilo kuna sanamu kubwa ya mwanamke aliyepanda farasi akiwa nusu uchi.Uwazi wa kiti hicho umezua maswali mengi hasa kwa wachambuzi wa Biblia kutokana na Biblia kutamka wazi katika UFUNUO 13 kuwa namna 666 ni ya mpinga kristo.Wachambuzi wa Biblia wanasema umoja wa ulaya ni moja kati ya maeneo ambayo yanaharakisha ujio wa mpinga kristo.


Viongozi wa serikali na Dini wajadili Amani Tanzania

Viongozi wa serikali, dini, na taasisi mbalimbali nchini wiki iliyopita wamekutana kwa siku mbili ili kujadili mambo mbalimbali yatakayodumisha AMANI na Umoja wa watanzania.Mkutano huo ulifanyika katika Hotel ya White Sands ya jijini Dar es salaam na kufunguliwa na Makamu wa Rais Mh Mohamed Gharib Bilal ambaye aliwaasa viongozi wa didi kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza na kulinda umoja wan kitaifa na kusaidiana katika kukemea vitendo vya kifisadi.

Kwa mujibu wa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of GOD(TAG) Askofu Barnabas Mtokambali ambaye alihudhuria kikao hicho alisema “ kikao hiki kimejenga msingi wa utatuzi wa matatizo ambayo yanaweza kuondoa Amani ya nchi yetu”

Mawaziri waonywa Ikimbieni hukumu ya Mungu
Mawaziri wenye tuhuma mbalimbali zinazowagusa wao binafsi au kushindwa kutekeleza wajibu wao na kusababisha uchungu na mateso makali kwa watu masikini na wale wenye kipato cha chini huku kukiwa na tishio la kutoweka kwa amani kutokana na kukithiri kwa tuhuma za ufdisadi na rushwa.

Wito huo umetolewa na viongozi wa dini na wabunge mbalimbali waliohojiwa na gazeti la jibu la Maisha katika nyakati tofauti tofauti.Akiongea kwa kujiamini Mbunge wa Iringa mjini Piter Msigwa alisema kuwa yeye alishiriki katika kamati ya bunge iliyokuwa ikichunguza tuhuma zilizokuwa zinamkabili waziri wa maliasili na utalii Mh Ezekiel Maige na alioyaona huko yanatisha kwa kuwa Mungu huwa na tabia ya kuchoka na kushusha hukumu yake kwa muhusika.

Msigwa ambaye pia ni Mchungaji alisema, nchi haiko salama kuliko unavyodhani, kwa kuwa kuna watu wengi walipaswa kufanya jambo kuliokoa taifa lakini bado hawajafanya. Wakati umefika kwa viongozi wa dini kujitenga na pesa zinazoletwa makanisani na watuhumiwa wa Ufisadi na tuwe makini kama nabii Mika kwa kuwaambia hapana.

Alisema kama viongozi wa dini wakisimama wakakataa wanasiasa mafisadi wanaojaribu kukimbilia kanisani kujisafisha kwa fedha chafu, wanachi hao wakisimama imara na kusema wizi, basi na wanasiasa wema waliosalia wakavunja nira na mafisadi nchi itasalimika.


Kutoka gazeti la Msemakweli

Pope Benedict
Mkuu wa wakatoriki duniani atangaza maisha yake kufikia ukingoni
Kiongozi wa kanisa katoriki duniani Papa Benedict XVI amesema kwamba hivi sasa anakaribia mwisho wa maisha yake katika umri wa miaka 85 alionao, lakini anauhakika kwamba Mungu atamsaidia katika kufanya kazi zake za Kitume.Kauli hiyo isiyotarajiwa imetolewa na kiongozi huyo wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa jijini Vatiokani nchini ITALIA yalipo makao makuu ya kanisa hilo duniani.

VCC Pastors fellowship kuandaa mkutano mkubwa jijini Dar es salaam
Huduma ya Pastors Fellowship inayoongozwa na kanisa la Victory Christian Centre  lililo chini ya Mch Huruma Nkone, limefanikiwa kutimiza maono yake baada ya kukusanya wachungaji mia tano wa mikoa ya Pwani na Dar es salaam.Ushirika huo wa wachungaji ulikutana katika ukumbi wa Hotel ya Landmark ya jijini Dar es salaam na moja kati ya mikakati yake ni kuandaa mkutano mkubwa utakaofanyika katika viwanja vya Jangwani mnamo mwezi sita mwaka huu wa 2012.


Gazeti la Nyakati

Mchungaji Masanja asema wanaoruhusu wanawake kuvaa suruari kanisani wamepotoka
Mchungaji Gervas Masanja wa kanisa la Pentekoste Mission Church la nchini Tanzania akiongea na Gazeti la Nyakati baada ya kuulizwa kama kuna tatizo lolote la kimaadili kwa mwanamke mkristo kuvaa suruali ibadani,Mch Masanja alijibu kama ifuatavyo “Kuvaa suruali kwa Mwanamke ni dhambi, Mapokeo na utandawazi vimewapoteza wengi, watumishi wanaowaruhusu waumini wao kuvaa suruali haijalishi ni kanisani au popote, hao sio watumishi wa Mungu mtu awe tayari kuwa na Bwana wakati wote. 

Wasabato masalia wataka waombwe radhi
Wachungaji watatu waliojitenga na kanisa la sabato(SDA) na kuanzisha kanisa linalojulikana kama Seventh Day Reformed  Remnants maarufu kama Wasabato Masalia wameutaka uongozi wa kanisa la SDA kuwaomba radhi vinginevyo watawapleka mahakamani..Hatua hii imekuja baada ya Kanisa la SDA kuwafungukia mashitaka viongozi wa masalia kwamba wamedurufu vitabu vya mwanzilishi wa kanisa la SDA Nabii Ellen White pasipo idhini ya Nabii 

Picha Yetu Jumatatu Hii:Mtumishi Emmanuel Mabisa akiwa pembeni ya gari la mmoja wa Ma-Wise Men wa huduma ya SCOAN


Pichani ni Kiongozi wa Glorious Celebration Emmanuel Mabisa akiwa pembeni mwa gari la mmoja wa ma- wisemen wanaotumika sambamba na Nabii Tb Joshua mwezi huu 4/2012.Mabisa na  Rulea Sanga walipata mwaliko wa kufika kanisani hapo kutoka kwa Nabii Tb Joshua.

Sunday, April 29, 2012

Emmy Kosgei,Sarah K, Christina Shusho, Waibuka kidedea katika Groove Awards 2011/2012



Sarah K na Esther wahome wakifurahia tuzo ya Sara K, hii ni baada ya Sarah K kuchukua Tuzo ya nyimbo bora ya kuabudu kupitia nyimbo yake ya LISEME

 
Tuzo Maarufu za Groove Awards 2011/2012 zimemalizika jana usiku nchini Kenya mabapo Mwanamuziki Christina Shusho kwa mwaka wa Pili mfululizo ameibuka kuwa mwanamuziki bora wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania. Katika tuzo hizo ambazo mwanadada Kambua Manundu na Uche agu ndio walikuwa washereheshaji(ma Mc) huku tuzo hizo zikienda sambamba na performance kali kutoka kwa wanamuziki mbalimbali wakiwemo

Uche-Agu(Double Double) kutoka South Afrika
Anthony Faulkner kutoka Marekani
Kambua Manundu
Emmy Kosgei
Jimmy Gait

Emmy Kosgei aibuka na tuzo mbili Mwanamuziki bora wa kike nchini Kenya huku album yake ya OLOLO ikichaguliwa kuwa album Bora ya mwaka.
Kambua aibuka mwandishi bora wa mwaka huku nyimbo ya Sara K iitwayo LISEME imeibuka kuwa nyimbo bora ya Kuabudu kwa mwaka 2011/2012

Katika sherehe hizo zilizodhaminiwa na kampuni ya simu ya Safaricom chini ya Safaricom skiza brand, zilikuwa zikirushwa LIVE na kituo cha television cha KTN pamoja na kwa njia ya mtandao.

Washindi wengine wa Groove Awards 2012 Winners wana alama Nyekundu


MALE ARTIST OF THE YEAR
Daddy Owen
Eko Dydda
Holy Dave
Jimmy Gait
Juliani
Man Ingwe


Emmy Kosgei akipokea moja ya tuzo yake na pembeni ni timu yake ambayo amekuwa akiimba nayo sehemu mbalimbali

FEMALE ARTIST OF THE YEAR
Emmy Kosgei
Gloria Muliro
Kambua
Mercylinah
Mercy Wairegi
Sarah Kiarie

GROUP OF THE YEAR
Adawnage
B.M.F
Kelele Takatifu
M.O.G
Maximum Melodies
Tetete

NEW ARTIST/NEW GROUP OF THE YEAR
Dan Gee
Everlyne Wanjiru
Kelele Takatifu
Maximum Impact
Willy Paul
Zipporah Eric

SONG OF THE YEAR
Exponential Potential – Juliani
Furifuri – DK & Jimmy Gait
Ghetto – Ekodydda
Liseme – Sarah K
My call – MOG
Ololo – Emmy Kosgei

Sara K akiongea mara baada ya kupokea tuzo ya Nyimbo bora ya Kuabudu kupitia nyimbo yake ya LISEME

WORSHIP SONG OF THE YEAR
Liseme – Sarah K
Nakutazamia – Mercy Wairegi
Niongoze – Mercylinah
Nisizame -Tumaini
Umetenda mema – Kambua
Waweza – Everlyn Wanjiru

ALBUM OF THE YEAR
Ebenezer – Mercylinah
Kibali – Gloria Muliro
Liseme – Sarah k
Ololo – Emmy Kosgei
Pulpit kwa Street – Juliani
Utamu wa maisha – Daddy Owen

Uche agu ama uche Double Double akiongoza sherehe hizo kama Mc na pia aliimba

AUDIO PRODUCER OF THE YEAR
Billy Frank
Gittx
Jacky B
John Nyika
Papa Emile
Saint P

VIDEO PRODUCER OF THE YEAR
Eagle Films
Eyeris
J Blessing
Prince cam
Sakata
Washamba Unlimited

VIDEO OF THE YEAR
Exponential Potential – Juliani
Holy Ghost fire – BMF
My Call – MOG
Safari – Adawnage
Umetenda Mema – Kambua
Am Walking – Alemba & Exodus

Emmy kosgei akiwa na moja ya tuzo zake alizopewa

COLLABO OF THE YEAR
Fresh and Clean – Kevo Juice& Jimmy man
Furifuri – DK &Jiimmy Gait
My call – MOG & Julaini
Ni msoo – Kelele Takaifu & Holy Dave
Am Walking – Alemba & Exodus
Welwelo – Mr Seed& Danco

RAGGA/REGGAE SONG OF THE YEAR
Birthday – BMF
Fill me – Mr T & Samukat
Love came me way – Verbal
My Call – MOG Ft. Juliani
Number 1 – Kevo Yout
Am Walking – Alemba & Exodus

DANCE GROUP THE YEAR
Alabaster
Altamin
Detour
Iced
Saints
Zionists

GOSPEL RADIO SHOW OF THE YEAR
Gospel Sunday – Milele FM
Pambazuka – Citizen Radio
Route 104 – Hope FM
Shangila – Hope FM
Trinity Connect – Homeboyz Radio
Tukuza – Radio Maisha


GOSPEL TV SHOW OF THE YEAR
Angaza – KBC
Crossover 101 – NTV
Gospel Garage – K24
Kubamba – Citizen TV
Tukuza – Radio Maisha
Rauka – Citizen TV

Esther Wahome akifurahi kwa kucheza ukumbini hapo

RADIO PRESENTER OF THE YEAR
Allan T – Homeboyz Radio
Amani Aila – Hope FM
Anthony Ndiema – Radio Maisha
Eudias – Radio Jambo
James Okumu – Hope FM
Mike Gitonga – Radio 316


CENTRAL SONG OF THE YEAR
Nissi – Lois Kim
Agiginyani – Shiro wa GP
Marurumi – Wakabura Joseph
Mahindi Momu – Charles King’ori
Munduiriri – Carol Wanjiru
Muturire – Jane Muthoni


RIFT VALLEY SONG OF THE YEAR
Bong’o Longit- Gilbert Chesimet
Inet kei- Lilian Rotich
Kamura Tanet – Edina Kosgei
Kararan Chamet – Moses Sirgoi
Narue Tengek- Gilbert Segei
Ololo- Emmy Kosgei

Kambua aliyekuwa Mmoja wa Ma Mc na pia alichukua tuzo ya Mwandishi bora wa nyimbo za Injili nchini Kenya 2011/2012

ARTIST OF THE YEAR (TANZANIA)
Bahati Bukuku
Bonny Mwaitege
Christina Shusho
Neema Mwaipopo
Neema Nushi
Rose Muhando


SONGWRITER OF THE YEAR
Kambua



Angalia Live Perfomance ya SARAH K akiimba LISEME ukumbini hapo

Saturday, April 28, 2012

Baada ya Kutoka Honeymoney, Kambua kusherehesha katika Groove Awards usiku wa leo.


Mwanamuziki wa nyimbo za injili na aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha RAUKA Kambua Manundu, usiku wa leo TAREHE 28,04.2012 anatarajia kuongoza sherehe za kutoa tuzo kwa wanamuziki wa nyimbo za injili nchini Kenya.Kambua ambaye kaTika siku za hivi karibuni Katika viwanja vya hotel ya  Windsor alifunga ndoa na Mch Jackson Mathu ambaye licha ya uchungaji Mathu pia ni mfanyabiashara mashuhuri nchini humo.

Baada ya kutoka kwenye fungate siku kadhaa zilizopita,usiku wa leo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Kambua kusimama mbele za watu akiongoza shughuli akiwa kama mama mtumishi.

Kambua Siku ya Harusi yake

Kambua akiwa na mumuwe Mch Jackson Mathu siku ya harusi yao

Kambua akiwa na mumuwe Mch Jackson Mathu

Prestige cars down there
 Groove Awards ni tuzo zinazoheshimika sana kwa upande wa Gospel nchini humo na Afrika mashariki na kati. Kwa mwaka huu tuzo hizi zimedhaminiwa na kampuni ya simu ya Safaricom chini ya brand yake ya Safaricom skiza tone.Wanamuziki wa injili kutoka Tanzania wapatao sita nao wapo katika mchakato huo na kwa pamoja wanawania tuzo ya mwanamuziki bora wa injili kutoka Tanzania.
 

Artist Of The Year (Tanzania)
26a. Bahati Bukuku
26b. Bonnie Mwaitege
26c. Christina Shusho
26d. Neema Mwaipopo
26e. Rose Muhando
26f. Upendo Nkone


Friday, April 27, 2012

Kufuatia Uvumi wa kuwepo dhahabu Madhabahuni,Uchimbuaji dhahabu kanisani wakwama



Zoezi la kuchimbua dhahabu inayodaiwa imefukiwa ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli (KKKT), Dayosisi ya Kusini Usharika wa Brandt wilayani Mbarali mkoani Mbeya, hatimaye limesitishwa kufuatia kutokea vurugu za wananchi na kuhatarisha amani hali iliyopelekea polisi kuingilia kati ili kuepusha ghasia zaidi.
Kusitishwa kwa zoezi hilo kuliamuliwa jana na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini, Isaya Mengele na imeelezwa kuwa shughuli hiyo itaweza kuendelea  ama kutokuendelea kadri uongozi wa kanisa hilo utakapojadili yaliyojiri katika zoezi hilo.

Mchungaji wa Kanisa la KKKT Usharika wa Brandt, Emanuel Lunda, akizungumza na NIPASHE iliyofika katika kanisa hilo lililopo kijiji cha Ihahi, alisema uchimbaji wa  madini hayo  uliokuwa ukifanywa ndani ya kanisa hilo karibu na madhabahu ulilenga kutafuta dhahabu ambazo kama zingepatikana  zingeuzwa na fedha zingetumika kujenga kanisa jipya la kisasa.

Alex Malasusa Askofu mkuu wa kanisa la KKKT nchini
Alisema kabla ya vurugu hizo kutokea na kutolewa amri ya kusitishwa kwa zoezi la uchimbaji, tayari walikuwa wamechimba urefu wa zaidi ya futi 10, lakini hakuna dhahabu iliyokuwa imepatikana.
Mchungaji Lunda alisema pia fedha hizo ambazo zingetokana na mauzo ya dhahabu, zingetumika kujenga nyumba ya mchungaji na ya Mwinjilisiti wa mtaa wa kanisa hilo pamoja na kuweka huduma ya umeme katka kanisa jipya ambalo lingejengwa kwa gharama ya Sh. milioni 40 ambayo ilikuwa imetathiminiwa.

Alisema tetesi za kuwepo dhahabu ndani ya kanisa hilo lililojengwa miaka ya 1905 na Wajerumani, kwa muda mrefu zilikuwa zikienezwa na baadhi ya wakazi wa kjijiji cha Ihahi ambapo Mkuu wa Jimbo la Chimala, Laulent Ng’umbi naye alidokezwa suala hilo ambaye naye aliwaeleza viongozi wa Dayosisi ya Kusini na hivyo ikaamuliwa ufanyike utafiti wa madini hayo kwa kuchimba ndani ya kanisa.

Alisema mwanzoni mwa Aprili mwaka huu uongozi wa Dayosisi, Jimbo na Usharika baada ya majadiliano ya suala hilo, waliitwa wataalam wa madini ambao walipima ndani ya kanisa kwa kutumia vifaa maalum vya kutafuta madini ambao walipima mara tatu kwa nyakati tofauti na kugundua  kulikuwa na madini ndani ya kanisa hilo.
Mchungaji Lunda alisema mara ya tatu wataalam hao walipofika katika kanisa hilo kwa ajili ya kupima madini hayo waliambatana na Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kusini, Mwamisole, Mkuu wa Jimbo la Chimala, Laulenti Ng’umbi, Mchungaji Mbilinyi wa Jimbo la Chunya na Mkuu wa Jimbo la Mtwara-Lindi, Mchungaji Mbedule.

“Ilipofika Aprili 18 niliitwa makao makuu ya Dayosisi Njombe ambapo Askofu Mengele wa Dayosisi ya Kusini, alinieleza kuwa suala la kuwepo dhahabu ndani kanisa la KKKT Usharika wa Brandt limejadiliwa kwenye mkutano mkuu wa Dayosisi na kwamba hakuna jinsi ni lazima utafiti ufanyike,” alisema Mchungaji Lunda.

Aliongeza kuwa kabla ya zoezi la kuchimba dhahabu ndani ya kanisa kuanza, kuliitishwa kikao cha wazee wa kanisa na viongozi ambacho kilihudhuliwa na wajumbe 14 wakiwemo wazee wa kanisa, wajumbe kutoka kamati ya majengo, idara ya vijana, idara ya wanawake na wazee maarufu wa kijiji cha Ihahi.

Alisema wajumbe wa kikao hicho walipendekeza kuwa wakati wa zoezi la kuchimba dhahabu ndani ya kanisa kuwe na usimamizi wa viongozi na waumini ili kusitokee ujanja wa kuibiwa madini na pia madini yatakayopatikana yauzwe na fedha zitakazopatikana zitumike kujenga kanisa jipya la kisasa, nyumba ya mchungaji, nyumba ya mwinjilisti na kuweka huduma ya umeme.

Mchungaji Lunda alisema siku ya Jumatatu Aprili 23, wachimbaji madini waliokuwa wametafutwa na kanisa walianza kazi kwa usimamizi wa karibu na Katibu Mkuu wa Dayosisi, Mwamisole, Mkuu wa Jimbo la Chimala, Ng’umbi Mkuu wa Jimbo la Mtwara-Lindi, Mbedule Mchungaji wa Usharika wa Brandt (Lunda) na Mwinjilisti wa Mtaa, Martin Msigwa.

Alisema zoezi la kuchimba dhahabu lilianza kati ya majira ya saa 7:00 na saa 8:00 mchana ambapo makubaliano ilikuwa kazi hiyo iwe inafanyika hadi nyakati za usiku, ilipofika siku ya Jumanne saa 12:00 jioni alikifika Mwenyekiti wa Kijiji cha Isitu aliyefahamika kwa jina la Mama Mkwembe ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Ihahi alianza kuhoji ni kwanini kanisa linachimbuliwa.
“Huyu Mwenyekiti wa kijiji cha Isitu alipokuja alianza kufoka na kueleza kuwa ninyi mna uroho wa utajiri na kutishia kutoa taarifa polisi lakini hakuna aliyemjibu kwasababu tulijua suala hili limefuata taratibu zote na kuruhusiwa na viongozi wa kanisa,” alisema Mchungaji Lunda.
Aliongeza kuwa baadaye Diwani wa kata ya Ihahi, Mtendaji wa kata ya Ihahi na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihahi nao walifika katika kanisa hilo lakini walipopewa maelezo ya jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa walilidhika na kukubali kuwa liendelee sababu limefuata taratibu zote za kanisa hilo.

Mchungaji Lunda alisema siku hiyo ya Jumanne majira ya  saa 6:30 usiku Mwenyekiti wa Kijiji cha Isitu akiwa na askari mmoja aliyetajwa kwa jina la Allen Mwamaja walifika katika kanisa hilo na askari huyo alianza kufoka kutokana na zoezi hilo na kisha kumnyang’anya simu ya mkononi na kuondoka nayo.

Kwa mujibu wa mchungaji huyo, ilipofika saa 8:00 usiku walifika askari wengine zaidi ambao waliingia ndani ya kanisa hilo na kuchukua kamera ya video, kamera ya kawaida, sururu, beleshi (sepetu), tochi, redio na viatu vya mmoja wa wachimbaji na kuondoka navyo hadi kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Chimala.
Mchungaji Lunda alisema kutokana na vurugu hizo, Askofu Mengele wa Dayosisi ya Kusini, alitoa amri zoezi hilo lisitishwe na shimo lifukiwe kazi ambayo tayari imekwishatekelezwa.

Hii ni mara ya kwanza kanisa kuchimbuliwa kusaka dhahabu inayodaiwa kufukiwa ndani yake. Ingawa maeneo mbalimbali nchini kwa sasa yanadaiwa kuwa na dhahabu hakuna kokote ambako inadaiwa kuwa yamefukiwa na mtu.

CHANZO: NIPASHE

Sikiliza Walichokisema Emmanuel Mabisa na Rulea Sanga baada ya kutoka Nigeria kwa Tb Joshua.



Emmanuel Mabisa na Rulea Sanga hivi karibuni walipata Bahati ya kupata Mwaliko maalumu kutoka kwa Nabii  Tb Joshua hasa baada ya Tb Joshua kuona Ghraphics Pictures ambazo Rulea Sanga alizifanya na kuziweka kwenye Blog yake iitwayo Rumaafrika.Watumishi hawa siku mbili zilizopita   wamerejea nchini kutoka Lagos Nigeria na Hosanna Inc ilipata nafasi ya kufanya mahojiano nao. 

Unaweza kuwasikiliza hapa chini juu ya safari yao nzima toka wanaondoka nchini hadi wanarudi.

Rulea Sanga akiwa katika uwanja wa ndege wa Ethiopia wakati wakielekea nchini Nigeria

Emmanuel Mabisa akiwa nchini Nigeria katika kanisa la Tb Joshua na hapa ni PRAYERS LINE ambapo Wise Men pamoja na Nabii TB Joshua hufanyia Maombezi



Wednesday, April 25, 2012

Package From Altar:Ushirika na Roho mtakatifu – Mwl Mgisa Mtebe



Huwezi kutawala mwili pasipo Roho,Roho ndiyo inatawala mwili, ulimwengu wa Roho ndiyo ulioumbwa kwanza na ulimwengu wa mwili ukafyatuliwa,kutoka ulimwengu wa Roho.

Baba anasema tufanye mtu, Mwana anakwenda kufanya mtu, ni Roho Mtakatifu anayekwenda kudhihirisha ule udongo wa tope unakuwa mwili, nyama,damu na mifupa mtu anakuwa nafsi hai. Ni baba anayesema mguse kipofu, ni Yesu anayemgusa kipofu , ni Roho mtakatifu anayerudisha golori kwenye macho ya kipofu.


Mwl Mgisa Mtebe

Rumi 8 :29
Usijilinganishe na mtu mwingine yeyote,jilinganishe na Kristo tafuta kufanana na Yesu, si sawa kabisa kujazwa na Roho Mtakatifu kisha ukawa mtu wa kawaida,
Kanuni za kawaida kabisa zikikugomea  lile gape la tarajio na uhalisia linapokuja unafanya nini, ulikuwa unatarajia hiki kikaja hiki kuna gape hapo,hapo ndipo unaingiza kitu kinaitwa gia ya Imani, unaaply the supernatural kwa kuwa NATURE imeku-dissapoint.Ulitegemea ukisoma utafaulu lakini kadri unavyoendelea kusoma matokeo yanazidi kuwa mabaya kuna gape hapo kati ya kusoma na matarajio.Sasa unalijazaje hilo gape hapo kati ya tarajio na hali halisi.Wewe umeokoka hutakiwi kuiba mitihani wala kuibia ukiwa katika chumba cha mitihani ili na baadaye uende mbinguni vile vile, usije ukapata “A”ukaenda jehanum.Palipo na gape kati ya tarajio na uhalisia ndipo gia ya imani huingia.

Kuna namna mtoto wa Mungu anaweza akaishi duniani bila kujichafua na akapingana na  changamoto zote za maisha ya kikristo na akashinda, akawa succsesfull duniani na mbinguni akaingia.Kuna kanuni zake, pale maisha yanapokuwekea gape ndipo unaingiza gia ya Imani. Kuna vitu vingi vinachangia katika uwezo wa mtu wa kiakili, kitaalamu intellingent quotient(IQ). Unataka kufaulu unataka kukumbuka, unakuta unaomba na unalala darasani kisha haufaulu, lakini wapo ambao kabla ya kwenda kusoma wanaenda vuta bangi.Matokeo yakija wao manapata A na wewe unapata ”C”  wakati na kunena kwa lugha unanena.

Tatizo la kiakili sio lazima liwe limechangiwa na mapepo, kitaalamu wataalamu wa saikolojia wanasema wakati baba yako na mama yako wanakutafuta walikuwa katika hali gani, kama walikuwa mawekasilishana, wanawaza madeni na matatizo, vile vichembechembe vinatengeneza makeup ya wewe baadaye, na hata wakati umetungwa mimba mama yako alikuwa katika hali gani, kama alikuwa mtu wa machozi,kukasirika, kulalamika hivyo vichembechembe viliingia, na alikuwa anakula chakula gani hilo nalo ni la msingi.

Na hata wakati unazaliwa ulikaa sekunde ngapi ukikosa hewa, kama ulikaa muda mrefu pasipo kuvuta hewa, uwezo wa kiakili hushuka.Hapo utaona uwezo wa kiakili hauchangiwi tu na mambo ya kiroho.Haya sasa umeshazaliwa katika mazingira hayo na uko first year unafaulu vipi? Ukijikuta katika hali hiyo ya kimasomo hapo ndipo Imani hutumika, wakati wengine wanatarajia ufeli lakini kwa imani unalijaza hilo gape na kufaulu
Unamawazo ya kuwa Lawyer, Accountant, daktari anakwambia moyo wako umechoka,au anasema una kansa ya damu,umetarajia biashara itaenda hivi inaenda hivi, maisha yanakufrastrate yanakutendea visivyo.Hapo ndipo NGUVU ya imani inapoingia kazini,kila mtu anaye kujua kiuchumi, kiakili anashangaa umefika vipi upande wa pili na umewaacha watu wote midomo wazi.

Yesu aliposema nyumba iliyojengwa juu ya mawe alimaanisha nini,yale mawe hayahitajiki siku zote yanahitajika siku ya Dhoruba na siku ya tetemeko,dhoruba isipokuja tetemeko lisipokuja aliyejenga juu ya mawe na juu ya mchanga hakuna tofauti,the only defference ni siku ya disaster.

Wakati wengine wanafaulu hali kwako inakuwa ngumu, usione kuwa kuendelea kusali ni kitu kama mzigo vile, wee endelea kuwekeza kwa kuwa kuna siku ya dhoruba.Tunajifunza haya mambo ili tuweze kupata kila kitu ambacho Mungu alitukusudia cha kutuwezesha  kuishi maisha ya ushindi na mafanikio duniani. Hatukuitwa kuteseka, hatukuitwa kushindwa, kufeli kuhangaika.Huwezi kufanikiwa katika ulimwengu huu pasipo kutumia nguvu fulani ya Kiroho.

Huwezi kutawala mwili pasipo Roho,Roho ndiyo inatawala mwili, ulimwengu wa Roho ndiyo ulioumbwa kwanza na ulimwengu wa mwili ukafyatuliwa/ ukazaliwa  kutoka ulimwengu wa Roho.Sio kwamba ulimwengu wa Roho uliumbwa kushoto ulimwengu wa mwili ukaumbwa kulia, ulimwengu wa Roho uliumbwa kwanza ulipokamilika  vilivyokuwa ndani ya ulimwengu wa Roho vikazaa ulimwengu wa mwili.

Hivyo ulimwengu wa mwili umetokea katika ulimwengu wa Roho,huwezi kutawala ulimwengu wa mwili, bila kupitia nguvu ya kiroho.Unahitaji nguvu za MUNGU,na Roho mtakatifu ndiye NGUVU YA MUNGU, ndiye anayewezesha kauli ya Baba na matendo ya mwana yanakuwa dhahiri. Baba anasema tufanye mtu, Mwana anakwenda kufanya mtu, ni Roho Mtakatifu anayekwenda kudhihirisha ule udongo wa tope unakuwa mwili nyama damu na mifupa mtu anakuwa nafsi hai. Ni baba anayesema mguse kipofu, ni Yesu anayemgusa kipofu, ni Roho mtakatifu anayerudisha golori kwenye macho ya kipofu.

Kwa kupewa Roho mtakatifu ni kukufanya uwe kama Yesu,kwa kuwa anakuambukiza uwezo aliokuwa nao Yesu.  1Yoh 4: 12-17 “Kama yeye alivyo na sisi ndivyo Tulivyo” Rum 8: 29, Efeso 4; 11-14.Mungu anataka uwe YESU Mdogo duniani, ufananishwe na mfano wa mwanawe, watu wote wanaomhitaji Yesu waje kwako kwa kuwa yeye alivyo ni kama wewe kwa kuwa umepewa Roho wake.

Itaendelea......
Mwl Mgisa Mtebe

Diana Madida Muimbaji mtanzania anayemtumikia Mungu nchini Uingereza



Diana Madida Kihayile
Diana Madida Kihayile ni jina jipya baada ya kuolewa mwaka 2006 na Mr Bubele E Kihayile.kabla ya hapo amekuwa akijulikana kwa jina la Diana Madida.Diana amezaliwa na kukulia jijini Mwanza Tanzania,kwa sasa anaishi jijini Birmigham nchini Uingereza.Yeye pamoja na mumewe Mungu amewajalia watoto wawili wa kike,Rina Jodiah mwenye miaka miwili, na Jaina Sasha mwenye miaka mitano, kwa sasa Diana pamoja na familia yake wanasali katika kanisa la El Shadai International christian centre la jijini Birmigham nchini Uingereza.

Kimasomo Diana toka kidato cha kwanza mpaka cha sita amesomea shule ya sekondari Mwanza, wakati akiwa mdogo alikuwa anashiriki katika michezo ya  utamaduni,ngonjera na kwaya ya shule.Pamoja na kushiriki kote huko lakini alikuwa bado  ni mtu mwenye aibu nyingi japokuwa alikuwa anasikia furaha sana pindi  akifanya kitu na watu wakafurahi.Ambition yake kubwa toka akiwa mdogo ilikua kuwa sister wa kanisani na mcheza netball.

Diana akiwa na mumuwe Bubere na mtoto wao
Diana alimpa Yesu maisha mnamo  june 1997 kupitia mkutano wa Dr Moses Kulola na kuanzia hapo akaamua kujiunga na kanisa la E.AG.T  IMANI  lililo chini ya  mchungaji Juliana Nyanda maeneo ya Pasiansi jijini Mwanza napo ndipo safari yake kihuduma ilipoanza rasmi.Mwaka 1998,Diana alijiunga na kwaya ya kanisa iitwayo FAITH AMBASSADORS ya kanisani kwao na baada ya muda alianza kuimbisha baadhi ya nyimbo. 

Mwaka 1999 aliendelea kukua kiroho na kihuduma akaanza kulead ibada za kusifu na kuabudu ndani ya kanisa hilo na mwaka 2000 alijiunga rasmi na Kihayile band.
Mwaka 2003 alitoa solo album aliyeipa jina la “MIMI NAJUA KWAMBA YESU ANANIPENDA” na ilisambazwa na MAMU. Baada ya kutoa album hiyo mwaka uliofuatia yaani 2004 baada ya kumaliza kidato cha sita  Diana aliondoka nchini na kuelekea jijini Birmingham kuendelea na masomo ya juu hivyo Mamu hakuendelea tena kuisambaza album hiyo.  

Diana on stage
 Alipofika nchini Birmingham Diana aliendelea na huduma ya kusifu na kuabudu katika kanisa la Lighthouse chapel. Mwaka 2008 kwa msaada wa Mumewe Mr. Bubele aliweza tena kutoa album ya pili  aliyoiita MILELE, album hiyo  ilikuwa na nyimbo kama Uwe karibu nami,Tumeahidiwa ufalme mwema na milele iliyobeba jina la Album.Album hii Diana aliingiza sokoni nchini Uingereza na aliweza kuituma nyumbani kwenye baadhi za vituo vya redio.

Baada ya hapo,Diana M Kiyahile  aliweza kuunganisha plan zake kihuduma na mumewe ambapo ni jambo la kumshukuru Mungu kwani  kwa mujibu wa Diana mwenyewe anasema “naamini mmoja anaweza ua elfu ila wawili makumi elfu.Mr bubele Kihayile is the perfect match from heaven to me,ni mentor wangu,mwalimu wangu,mtunzi wa nyimbo na muziki wote wa nyimbo zetu na mtumishi mwenzangu katika huduma”. Kwa sasa wana kihayire hao wanesharekodi nyimbo nne kati ya hizo wamerekodi video moja ya wimbo unaitwa Africa yetu.Kwa kipindi hiki Bubere na Diana wameanzisha  huduma iitwayo Diana & Bubele Music ministries na kwa sasa wanaanda album ya kwanza ikiwa kama  huduma kamili.

Marajio yao  makubwa ni kuona ufalme wa Mungu umetukuka duniani na wanasisitiza “we are created to worship and to usher his people into his presence. Ni matarajio yetu kuongeza uamsho wa kusifu na kuabubu kwanza nyumbani kwetu Tanzania,Africa na duniani kote kwa ujumla,pia kwa kutumia muziki wa Africa kuleta uamsho ndani na nje ya afrika yetu.kwa kuwa Mungu ametupa instrument ambayo ni sauti na utunzi wetu tutaitumia kuyafanya mapenzi yake popote na kwa vyovyote atakavyo tuongoza,hatimaye tungependa tuwe mfano na daraja kwa watumishi wenye wito kama huu” 

Mr and Mrs Bubere Kihayire
Hosanna Inc: Ni Changamoto gani ambazo mtu aliyeokoka anakutana nazo akiwa Uingereza ambazo asingeweza kuzikuta akiwa Tanzania?
Diana:Mhh,kikubwa ni kubalance muda wa maisha kwa ujumla na huduma,kwa hapa kila mtu yuko na wajibu wa kufanya kazi na kuedesha maisha yake ambapo unakuta kila saa counts.Maisha ya UK kwa ujumla yanahitaji commitment ambapo ili uweze kuwa sawa na kusurvive inabidi uwe na descpline ambapo ni tofauti na Tanzania.Unaweza ukawa na muda wa kutosha kwenye huduma na maisha yakaendelea kawaida,ila nisikufiche kwa hapa there is no chance ya kwenda church five times a week! kama nilivyokuwa nafanya Tanzania.

Hosanna Inc: Artist gani wa injili ambaye kwa muda mrefu umekuwa ukimfatilia na amekuhamasisha sana katika kumtumikia Mungu?
Diana:Nimekua namsikiliza Cece winans kwani ni mwanamke ambaye naamini ni kipenzi cha Mungu,anampresent Mungu katika uzuri na utukufu wake kwa kina kinachoigusa mioyo ya wasiliklizaji wa nyimbo zake.Pia Yolanda adams ni kiboko kwa kuitumia sauti yake kumtukuza Mungu.

Wito wake kwa kanisa la Tanzania
Ni vyema kuishi maisha yanayomwabudu Mungu,na kuedelea kuuboresha uhusiano wa mtu na Mungu mbali na huduma anayomfanyia Mungu,watumishi wengi wanasahau kuwa huduma sio uhusiano,pia inapokuja kwenye huduma wasidharau calling walizonazo na kutamani za wengine,kile Mungu alichomwekea mtumishi ndo portion yake na ukikitendea kazi Mungu atapanua hema yako na maisha yako yatakamilika.


Her  Favourite Colour.
White/Cream
Inaonyesha usafi na ni rahisi kuspot uchafu,pia inapendeza.

 Nje ya Huduma ya uimbaji Diana ni
Mwinjilist mwalimu wa watoto(suday school)


What is ur Favourite Gospel Song kwa Tanzania
Unajibu maombi-Upendo Kilahiro
Her Favourite Gospel Song nje ya Tanzania
My redeemer lives (Nicole C Mullins)


What is your Favourite Gospel Hym{Tenzi}
Bwana Mungu nashangaa kabisa .

Her Favourite Bible verse
Mathew 7:7
Ombeni nanyi mtapewa,tafuteni nanyi mtaona,bisheni nanyi mtafunguliwa,
God has been faithful to me tangu nimeokoka nimeusimamia huu mstari na ninaendelea kuona matunda makuuubwa sana.



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...