Wednesday, October 12, 2011

Tofauti Ya Zaka Na Dhabihu - Mwl C.Mwakasege


Mwl Christopher Mwakasege
Kutokutoa zaka na dhabihu ni kumwibia Mungu. Mtu aliye mkristo asipotoa zaka na dhabihu anaitwa mwizi. Kuna wakristo ambao ni wezi lakini wao hawajui yakuwa ni wezi. Wamemwibia Mungu zaka na dhabihu. Mungu anasema hivi: 

             “Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia ZAKA na DHABIHU” (Malaki 3:8) 

            Kati ya amri tulizopewa na Mungu ni kwamba tusiibe. Kuiba ni dhambi. Na dhambi ina adhabu yake. Popote palipo na dhambi, laana hutokeza. Kwa wale wanaomwibia Mungu kwa kutokutoa zaka na dhabihu, wamefunikwa na laana. Ndiyo maana Mungu alisema hivi:

                “….. Mmeniibia Zaka na Dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana;   maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote  (Malaki 3:8b, 9).
            Laana maana yake ni kutokufanikiwa, kutofaulu, kutokustawi, kukosa furaha, kukosa amani, na kukosa mwelekeo sahihi. Ni wazi kuwa wakristo wengi hawana furaha, hawana amani na hawafanikiwi katika maisha yao ya kila siku, kwa sababu hawamtolei Mungu zaka na dhabihu. 

            Unapokosa kumtolea Mungu ili ujenzi wa nyumba yake – kanisa uendelee, Hagai 1:6 anatuambia Mungu anasema hivi;

            “Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka”. 

Zaka ni kitu gani?
              Zaka ni fungu la kumi la pato lako. Hebu isome na kuitafakari mistari ifuatayo;
             “Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana ….Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; SEHEMU YA KUMI watakuwa ni watakatifu kwa Bwana” (Mambo ya Walawi 27:30 –32).

            “…Toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako,  akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo”(Kumbukumbu la Torati 14:28-29). 

            Zaka ni fungu la kumi la pato toka mshahara wako ofisini, shambani au kwenye mifugo. Tena zaka hii ni ya Bwana na ni Takatifu.
                    Mtu asipoitoa zaka hii anamwibia Mungu. Zaka si yako hustahili kukaa nayo wala kuitumia nje ya utaratibu wa Mungu. 


                    Lakini Malaki 3:10a anasema; “Leteni zaka KAMILI ….” Maana yake nini maneno haya? Maana yake ni hii; ikiwa kwa mfano mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/= ( kabla ya makato) – fungu la kumi au zaka unayotakiwa kutoa ni shilingi 200/= ambayo ndiyo zaka kamili ya mshahara wako. Ukileta pungufu yake hiyo si zaka kamili.
                         Tena kwa mfano umevuna magunia 10 ya mahindi toka shambani mwako – zaka kamili unayotakiwa kutoa ni gunia moja bila kupungua. Kumbuka mzaliwa wa kwanza wa mifugo yako ni wa Bwana. 

                        Unaweza ukasema habari za kutoa zaka ni za agano la kale na siyo za agano jipya.
            Waebrania 7:5-10 inatuambia wazi ya kuwa Ibrahimu alitoa fungu la kumi. Kama Ibrahimu alitoa sehemu ya kumi, Je! si zaidi sana kwetu sisi tulio uzao wake kwa imani ndani yake Kristo? Maana imeandikwa hivi;

            “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ahadi” (Wagalitia 3:29). Soma pia Wagalitia 3:13,14). 

Dhabihu ni kitu gani?
            Dhabihu ni matoleo yanayotolewa baada ya kutoa sehemu ya kumi ya pato lako. Kwa mfano, kama mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/=, basi sehemu ya kumi (zaka) ni shilingi 200/=. Kiasi cho chote utakachotoa ju ya shilingi 200/= ndiyo matoleo yako. Kwa mfano ukitoa shilingi 210/= toka kwenye mshahara wako wa shilingi 2000/=, Basi, shilingi 200/= ni zaka; na shilingi 10/= ni dhabihu au matoleo au sadaka ya kawaida.
            Kiasi utakachotoa katika dhabihu/matoleo, ndicho kitakachokuwa kipimo kitakachoweka kiwango chako cha kupokea. Imeandikwa hivi:

            “Lakini nasema neno hili, APANDAYE HABA ATAVUNA HABA; APANDAYE KWA UKARIMU ATAVUNA KWA UKARIMU. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, MKIWA NA RIZIKI ZA  KILA NAMNASIKUZOTE,mpatekuzidisanakatikakilatendojema;kamailivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye ATAYAONGEZA MAZAO YA HAKI YENU, MKITAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE MPATE KUWA NA UKARIMU WOTE; umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. 

Maana utumishi wa huduma hii HAUWATIMIZII WATAKATIFU RIZIKI WALIZOPUNGUKIWA TU, Bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, WANAMTUKUZA MUNGU kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote” (2Wakorintho 9:6-13)

            Soma tena mistari hiyo hapo juu, lakini sasa tafakari zaidi maneno niliyoyaandika kwa herufi kubwa. Utaona kuwa usipokuwa mwaminifu katika utoaji, wewe mwenyewe unakosa kufanikiwa, na pia unamkosesha Mungu shukrani na utukufu ambao angepata kwa utoaji wako. 

Zaka na dhabihu zitolewe wapi?
            Hili jambo linahitaji uongozi wa Roho Mtakatifu, ili upate ufahamu Mungu anataka upeleke wapi zaka na matoleo uliyo nayo.
            Hili ni muhimu kwa kuwa Biblia inazungumza juu ya kupeleka kanisani (Malaki 3:10-11), kwa watakatifu (2Wakorintho 9:12), kwa maskini (2Wakorintho 9:8-9), kwa watumishi wa Mungu (1Wafalme 17:10-24; 1Wakorintho 9:7-14); kwa wajane, - na kadhalika.
                Muombe Mungu akuongoze mahali pa kupeleka. Amani ya Kristo na iamue moyoni mwako. 

Baraka Tele!
            Kuna baraka tele za mafanikio kwa mkristo aliye mwaminifu katika kumtolea Mungu zaka na matoleo. 

            Katika Malaki 3:10 imeandikwa hivi; “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo (YA UTOAJI) asema Bwana wa Majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na KUWAMWAGIENI BARAKA, HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA AU LA”
.
             Je! umewahi kukutana na mkristo ambaye anashuhudia kuwa Mungu amempa baraka nyingi hata HANA MAHALI PA KUZIWEKA? Ni wazi kuwa ahadi hii haijatimia kwa kuwa hatujawa watendaji na Neno kikamilifu katika utoaji. 

              Soma mistari hii hapa chini uone baraka zingine zinazotokana na utoaji; “Azaria Kuhani Mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa Bwana, tumekula na KUSHIBA NA KUSAZA TELE; kwa kuwa Bwana amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa. Ndiko Hezekia akaamuru kutengeneza vyumba nyumbani mwa Bwana; wakavitengeneza. Wakayaingiza MATOLEO na ZAKA na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu ….” (2Mambo ya Nyakati 31:10-12). 

            Kwa nini wakristo wengine wanapungukiwa vyakula, wakati tuna nafasi ya kumruhusu Mungu kutubariki kwa vyakula tele? Mpe Mungu nafasi ya kukubariki kwa kumtolea zaka na matoleo! 

Anza Sasa!
             Nakushauri ya kuwa kama ulikuwa hutoi sehemu ya kumi au zaka pamoja na  matoleo ya kutosha – anza sasa.
             Jambo la kwanza, kumbuka kutubu kwa Mungu katika Jina la Yesu Kristo kwa kuwa ulimwibia zaka na dhabihu kwa kutokumtolea.
            Halafu mwombe Mungu akuwezeshe kusimama katika uaminifu wa kumtolea zaka na dhabihu ili apate nafasi ya kukubariki zaidi kama tulivyoona, na kama alivyoahidi.

Mwl Christopher Mwakasege.

38 comments:

  1. MUNGU Atusaidie sana tusisahau kumtolea zaka
    kwa mafundisho haya mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  2. Je? Kama kumtolea mungu zaka Na dhabihu nihali mungu alizungumza mambo haya katka kuonya kwake Sasa Vip Leo isaya 66:1-5.

    ReplyDelete
  3. Je? Kama kumtolea mungu zaka Na dhabihu nihali mungu alizungumza mambo haya katka kuonya kwake Sasa Vip Leo isaya 66:1-5.

    ReplyDelete
  4. Je? Kama kumtolea mungu zaka Na dhabihu nihali mungu alizungumza mambo haya katka kuonya kwake Sasa Vip Leo isaya 66:1-5.

    ReplyDelete
  5. bwana yesu asifiwe!
    ningependa kujifunza juu ya fungu la kumi.. kwa dunia ya sasa tunasema fungu la kumi ni baada au kabla ya makato ya kiserikali yaani fungu la kumi hesabu yake hutoka kwenye net salary au gross salary?

    ReplyDelete
    Replies
    1. mbona ameeleza vizuri hapo juu...soma makala haya vizuri utaeplewa mppendwa

      Delete
  6. ubarikiwe sana leo nimejifunza kitu muhimu sana......amani ya BWNA iwe kwetu sote AMINA

    ReplyDelete
  7. to me hata usipoipeleka zaka kanisani, hekaluni au kwa makuhani, ukiwapa yatima, wajane and the needy in general kwa uaminifu wote ni sawa na kumpa Mungu tu, Kanisani peleka dhabihu ndipo ili walawi wspate chakula hapo utazidishiwa kwa kushindiliwa na kusukwasukwa🙏

    ReplyDelete
  8. Bwana Yesu asifiwe je ni halali kutoa zaka kwenye pesa ya ada na mkopo?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nafikiri sio sahihi maana kwa kihasibu mkopo sio mapato wala school fee kwa mwanafunzi sio mapato pia.

      Delete
    2. So sisi tunaopokea boom chuoni , ile hela si ni mkopo, kwamaana hiyo unataka kusema tunakosea tunapoitolea fungu la kumi

      Delete
  9. Praise be to Jesus 4 his servant... I'm truly blessed

    ReplyDelete
  10. Kwa mnaouliza maswali soma pata ufahamu ndipo uliza mfano unknown anauliza kitu kilichojibiwa anajijibu tena jitahidini sana pata maarifa uliza utajibiwa vizur... Mungu jina lake litukuzwe Kwa mafundisho haya MITHALI 4:5,7 JIPATIE HEKIMA, JIPATIE UFAHAMU USISAHAU; NAAM KWA MAPATO YAKO YOTE JIPATIE UFAHAMU

    ReplyDelete
  11. Kwa mnaouliza maswali soma pata ufahamu ndipo uliza mfano unknown anauliza kitu kilichojibiwa anajijibu tena jitahidini sana pata maarifa uliza utajibiwa vizur... Mungu jina lake litukuzwe Kwa mafundisho haya MITHALI 4:5,7 JIPATIE HEKIMA, JIPATIE UFAHAMU USISAHAU; NAAM KWA MAPATO YAKO YOTE JIPATIE UFAHAMU

    ReplyDelete
  12. Asante mtumishi kwa somo zuri,Je kama ikatokea mtu amejikutà katumia mshahara wake akidhani bado balance inatosha,alipohesabu ili atoe zaka akakuta haitoshi tena,imeshamegwa na kutumika.Je mtu huyo anatakiwa afanyeje? Je kuna faini kwa ajili ya kuruka au kuchelewesha zaka ya mwezi huo?

    ReplyDelete
  13. Haleluya! Asante Bwana kwa neno hili lililo jema machoni pako. Asante Mungu kwa kunionya juu ya "mshahara kabla ya makato". Ni neno lililo kuu kwangu katika ujumbe huu wa neno la Mungu. Amen!

    ReplyDelete
  14. Je pesa ya kupewa na mzazi au mume kama matumizi waweza kutoa fungu la kumi hapo?

    ReplyDelete
  15. Je pesa ya kupewa na mzazi au mume kama matumizi waweza kutoa fungu la kumi hapo?

    ReplyDelete
  16. Nimebarikiwa kwa mafundisho asante sana

    ReplyDelete
  17. Nimekuelewa kabisa baba hv Kama nilitoa limbuko mfano ni mtoto wa kwanza afu ikatokea akafa natoa tena au

    ReplyDelete
  18. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  19. Shalom...ni. barikiwa sana hakika ila swali ni.. Kama ni mchungaji anapata pesa kwa kazi za mikono yake ni sawa akitumia fungu la kumi lake kununua au kutengenezea vifaa vya kanisani???

    ReplyDelete
  20. Nina swali hapo malimbuko na zaka .
    Zaka nimeelewa na dhabihu je malimbuko ? Msaada tafadhali

    ReplyDelete
  21. Je tunaweza kupata msisitizo wa utoaji zaka kwenye Agano jipya?

    ReplyDelete
  22. Ee Mungu Baba naomba msamaha kwa kuwa mwizi wa matoleo yako siku zote kabla sijapata somo hili naahidi kujitoa kwako ktk matoleo yote zaka dhabihu na fungu la kumi Kama Neno lako lilivyoandikwa katika Malaki 3:10 :leteni Zaka Kamili ghalani ili kiwemo chakula katika nyumba yangu.

    ReplyDelete
  23. Asante sana kwa mafundisho mazuri,Mungu atusaidie kuwa watendaji wa NENO.

    ReplyDelete
  24. Mungu akubariki Mwalimu kwa kutufundisha haya.

    ReplyDelete
  25. Mbona uyu mwalimu moongo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tafadhali, usimwite mwalimu wangu muongo. Kwahiyo unataka kusema Mungu ni muongo, 🙄🤔

      Delete
  26. Agano la kale limekwisha hii no NEEMA NAKWELI

    ReplyDelete
  27. ✍️🙏 humbled

    ReplyDelete
  28. Amen NIMEFANYIKA UPYA 🙏🏼🙏🏼

    ReplyDelete
  29. Mungu akubariki Sana Mtumishi wa Mungu Kwa mafundisho mazuri Mungu atusamehe na pia atuwezeshe tutende Neno lake jinsi lilivyo.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...