Home

Thursday, January 13, 2011

MTUMISHI CHARLES CHINCHIBELA ACHAGULIWA KUA NAIBU MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA

Mh Charles Chinchibela wa kwanza kushoto akifuatilia uchaguzi ulivyokua ukienda
 
Wakati alipokua akizunguka mashuleni na kuhudumu Neno la MUNGU kwa vijana wa Ukwata alikua akisema “siku moja ntakuja kua mwanasiasa mkubwa, napenda kuja kua mbunge”. Wengi wa wanafunzi walikua wakicheka lakini yeye alimaanisha. Amehubiri na kufungua matawi ya Ukwata  mengi katika jiji hilo na alwahi kuwa mwenyekiti wa ukwata mkoa pindi alipokua akisoma Mwanza sec.

Tarehe 5/1/2011 katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Mh charles Chinchibela diwani wa kata ya Mahina kupitia chadema alichaguliwa kushika wadhifa huo na kuapishwa tare10/1/2011.Charles maarufu mashuleni kwa jina la Chinchi alimshinda mpinzani wake toka cuf.Haikua nyepesi kwa Chinchibela kufika hapo kwa kua Mwaka 2000 na 2005 aligombea udiwani wa kata hiyo lakini kura hazikutosha mpaka uchaguzi wa mwaka jana ambapo aliibuka kidedea.

MUNGU wetu hujibu mara atafutwapo kwa bidii (2Nyakat 7:14),na akijibu hujibu kwa kishindo kikuu. Cha msingi hapa kwenye safari ya kila mtu, lile ambalo MUNGU amekwambia ndani ulifanye wee lifanye kwa bidii na kwa uaminifu wote,
na katikati ya safari atatokea.Yeye alieianzisha safari yako atatokea na kuikamilisha.
Chumba cha Uchaguzi ambapo zoezi lilifanyika kwa utulivu
                                                                                     

No comments:

Post a Comment