Home

Friday, January 28, 2011

TUZO ZA MUZIKI WA INJILI TANZANIA ZARUDI TENA MWAKA HUU

Mtumishi Harris Kapiga mratibu wa Tanzania Gospel Music Promoters ambao ndio waandaaji wa tuzo hizo
Tanzania baada ya miaka mitano itashuhudia kufanyika  tena kwa Tuzo za muziki wa Injiri kwa Mwaka huu wa 2011.Tuzo hizo ambazo huratibiwa na Tanzania Gospel Music Promoters(TGMP) zinatarajiwa kufanyika jijini Dar-es-salaam Tar 27-Feb-2011. Akizungumza na waandishi wa habari katika utambulisho wa tuzo hizo, mratibu wa Tuzo hizo Ndugu Harris Kapiga ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za injili na mtangazaji wa Clouds Fm alisema mradi wa kutokomeza maralia yaani Zinduka ndio mdhamini mkuu wa tuzo hizo mwaka huu.
                                                                       
     Kwa mujibu wa Kapiga lengo kuu la tuzo hizo ni kuwapongeza na kuthamini kazi za waimbaji wa nyimbo za Injili hapa nchini. Nyimbo zitakazoingia katika mchakato huo ni zile zilizofanya vizuri katika mwaka uliopita.
                                                                                      
Ultimate Praise Africa Gospel Music Award  hizi nazo ni  Tuzo za Music wa Injiri zitolewazo nchini uingereza kuuenzi Muziki wa Injili toka Barani Africa
Tuzo  za muziki wa Injiri Tanzania kwa mwaka huu, zimegawanywa katika makundi yafuatayo

                                a) Msanii bora wa mwaka wa Kiume
                                b) Msanii bora wa mwaka wa Kike
                                c) Kwaya bora inayotumia vyombo vyote
                                d) Kwaya bora inayotumia piano pekee
                                e) Kwaya bora isiyotumi chombo chochote
                                f) Bendi bora ya Injili
                                g) Single bora ya msanii wa Kiume
                                h) Single bora ya msanii wa Kike
                                i) Msanii bora mpya wa kike
                                j) Msanii bora mpya wa Kiume
                                k) Mtayarishaji(Producer) bora wa Injiri
                                l) Mtengenezaji bora wa video za injiri
                               m) Balozi bora wa jamii
                               n) Kundi bora la mwaka


No comments:

Post a Comment