Home

Saturday, February 12, 2011

JIFUNZE KUMTEGEMEA MUNGU KATIKA MAAMUZI YAKO

Katika maisha yetu kila siku ni rahisi kufanya maamuzi kwa mazoea kwa kua ndivyo tulivyozoea au ndivyo tulivyozoeshwa. Biblia inasema "Tazama Mtu akiwa ndani kristo amekua kiumbe kipya 2kor2:17".Hivyo ikiwa maisha yanakua mapya hata mfumo pia unakua mpya. Kinachopelekea hali ya wakristo inakua tofauti na matarajio  ni pale mkristo anapoingia katika mfumo mpya ndani ya kristo huku akiishi kutumia mfumo wa maisha ya kale.Hapo utakua unaweka kiraka kikuu kuu katika nguo mpya isiyo na kasoro. Wagalatia 5:16 enendeni katika Roho wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili, kwa kua Mwili hutamani  kushindana na Roho,na Roho kushindana na Mwili…..
          Shida inakuja pamoja na watu wengi kujua umuhimu wa kuongozwa na Roho wa MUNGU, Bado wengi wetu hatujui huyu Roho wa Mungu anamuongozaje mtu.Kwa mfano utajuaje kua katika jambo unalotaka kulifanya ni Roho ndio anakuongoza kulifanya ama ni akili yako(utashi).Ikifikia hapo, wakristo wengi leo tunamashaka utaskia ooh ,sijui…,unajua ….kifupi hatuna uhakika ni kipi kiko nyuma ya maamuzi hayo tuliyoyafanya ama tunayotaka kuyafanya
Leo wakristo wengi hupenda kuongozwa na ROHO katka maamuzi yao ya kila siku,lakini hawajui namna ROHO amuongozavyo mtu

Biblia inatuonyesha njia kadhaa ambazo Roho wa Mungu huzitumia kuwaongoza watu wake.Pindi unapotaka kufanya jambo utasikia ndani yako uhuru au kufunguka, hii ni moja ya njia anayotumia Mungu kumuongoza mtu wake.Ikiwa unataka kufanya jambo kasha ukasikia uzito,mashaka au ugumu ndani yako hakuna hali ya kufunguka ndani juu ya hilo ujue hauko sahihi rudi na jipange upya katika Kristo.kwa nini iwe hivi?
             Kwa kua hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu… Warumi8;15”,hivyo ile hali ya hofu,ugumu,na kutokufunguka ndani pindi unapotaka kufaya au ufanyapo maamuzi fulani ni ishara kua MUNGU yuko mbali na hilo jambo. lakini mkiongozwa na  Roho hamko chini ya sheria Galatia 5:18”. Hampo chini ya sheria maana yake hamfanyi lolote kwa kulazimishwa ila kwa upendo wa kristo ulio ndani yetu unaotufanya tuwe huru kufanya bila hofu kwa kua kiini cha maaamuzi yetu ni Roho akaaye ndani yetu na sio utashi wetu wenye lengo la kutimiza tamaa za mwili

Upendo wa MUNGU kwetu ni mkuu (Great), na upo kutuongoza pindi tunapotafuta msada kwa MUNGU juu ya maamuzi yetu ya kila siku.
                                                                          
                                                                             

No comments:

Post a Comment