Home

Tuesday, February 15, 2011

MUNGU HUMPA ALIYE HODARI MSAADA

Popote mtu alipo Nguvu ya MUNGU huwapo uwanjani
Katika maisha ya wokovu baada ya mtu kuokoka tunaanza safari ya maisha mapya ndani ya kristo YESU. Ndani ya safari hiyo kuna vitu ambavyo MUNGU anakusubiria uvifanye ili yeye aje kukusaidia.Lipo tatizo ambalo pengine mtu wa MUNGU analo kabla hata hajaokoka hadi anaokoka na kukaa katika wokovu stil tatizo hilo anakua nalo. Hii haimaanishi kua MUNGU ameshindwa kulitatua au kapungua nguvu, bali MUNGU anamsubiria  aanze kufanya jambo Fulani katika Mungu ili yeye atokee.
       Popote mtu alipo Nguvu ya MUNGU huwapo uwanjani na shetani naye yupo uwanjani pia na majeshi yake, vyote vikimuwinda mwanadamu. Hivyo ufahamu wa mwanadamu humfanya au jenge ufalme wa Mungu au wa kipepo.kwa kua ki Biblia dunia na vyote viijazavyo nchi ni Mali ya Mungu. Hata upande wa giza uko chini Mungu        Zab 24.Pia tunamuona MUNGU akimuita Nebukadreza mtumishi wangu(Yer 27:5) pamoja na kwamba Nebukadreza alikua akifanya kinyume na MUNGU.
      Baada ya kuokoka ukaanza safari katika kristo kisha katikati ya safari ukaanza kufanya vitu vya KIMUNGU  kwa ulegevu wakati upande wa pili/giza wao wako serious wakifanya kazi zao kwa Nguvu automatically unakua mateka wao pindi ukitia mguu katika vita dhidi yao,nasi pia pindi tukifanya kazi ya Mungu kwa nguvu tunakua na nguvu dhidi yao tunapoingia vitani nao tunaibuka washindi nao wanakua mateka wetu. Hii ni kwa kua MUNGU hana upendeleo yoyote afanyaye kwa bidii humpa ushindi
Mdo 10:34.
Tunaposema tunamwabudu Mungu au kumtafuta MUNGU lazima tumaanishe kwa kua ibada hukaa katika mashindano na aliye hodari kiibada Mungu ndio humridhia
Kuyafikia yale malengo aliyonayo MUNGU juu yetu inahitaji bidii kwa kua hicho unachokitaka katika Kristo ili ukipate, mwanadamu huingizwa katika mashindano.Wakati wewe unakitaka upande wa pili nao hujipanga kinyume nasi,lakini MUNGU anabaki katikati kwakua anasema kwenye Zab 89 kua yeye “humpa hodari msaada”.Ina maana kama Mtakatifu leo akiwa nataka cheo kazini akafunga wiki akimlilia MUNGU,na ofisini hapo hapo akawepo mtu mwingine anahitaji cheo hicho hicho yeye akaenda kulala makaburini wiki na akamtoa mwanae kama sadaka  kwa kua Nuru na giza vyote ni vya Mungu hivyo Mungu atampa aliye hodari msaada. Hapa kwa mujibu wa biblia aliyeonyesha kumaanisha ndio MUNGU hua upande wake.
       Tunaposema tunamwabudu Mungu au kumtafuta MUNGU lazima tumaanishe kwa kua ibada hukaa katika mashindano na aliye hodari kiibada Mungu ndio humridhia.Hivyo kufanya ibada sahihi ni lazima turudi nyuma tuone baba zetu kina Ibrahimu,Isaka,Daudi walifanya nini nasi tujipange kwa kumaanisha.Mahali pasipo na Ibada sahihi pana utumwa na Mwanadamu ni kiumbe pekee kilichopendelewa na MUNGU kumfanyia ibada.Ni Matumaini yangu kua jamii ya watu wa MUNGU leo tubadilike na kumaanisha tunachokifanya kwa ajili ya MUNGU.

                                                                                 

No comments:

Post a Comment