Home

Thursday, March 31, 2011

Esther Wahome achaguliwa kua mwakilishi wa Uniliver Compay


Esther Wahome
Mwanamuziki wa nyimbo za injiri nchini Kenya Esther wahome amefanikiwa kupata mkataba wa mamillioni ya kikenya toka katika kampuni ya Uniliver inayotengeneza bidhaa mbalimbali za kufanyia usafi zikiwemo sabuni za Omo na Lifebuoy. Wahome atakua akifanya kazi kama balozi wa sabuni ya LIFEBUOY inayoendesha kampeni ya kuwaelimisha watoto wa shule juu ya umuhimu wa usafi kaika maisha yao ya kila siku. Kwa mujibu wa Uniliver kampeni hiyo chini ya Wahome ni ya mwaka mmoja na itazihushisha shule zipatazo themanini katika jiji la Nairobi na viunga vingine nchini humo. 

Hii ni changamoto kwa wanamuziki wa injili nchini Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla badala ya kusubiri kuitwa kwenye matamasha ambako wanakutana na watu waliookoka kwa sehemu kubwa, pia wanaweza kuandaa mpango kazi(Proposals) kwa ajili ya jamii na wakaweza kuifikia jamii kupitia washikadau wenye nia ya kufadhili mipango kazi hiyo.

Moja kati ya matangazo ambayo Esther ameanza kuyafanya kama sehemu ya mkataba wake na kampuni ya Uniliver
                                      

No comments:

Post a Comment