Home

Monday, April 25, 2011

Sowers kufanya Ziara nchini Australia


The Sowers Group
Sowers group ni kundi la Muziki wa Injili lililo maarufu sana katika Afrika mashariki na kati. Sowers linaundwa na jumla ya wanamuziki watatu ambao ni Mike Matumaini, Christelle Mugeni, Oswald Basoka,pamoja na Kosto Zahindai .

Mwezi ujao tarehe 23 May 2011 litakuwa likifanya ziara  nchini Australia yenye lengo la kumtukuza Mungu kupitia nyimbo zao mbalimbali. Sowers ni moja kati ya makundi machache toka Afrika ya mashariki yaliyopata Neema ya kufanya matamasha mengi nje ya Bara la Afrika. Sowers lenye asili yake nchini Rwanda kwa sasa linafanyia shughuli zake mjini Arusha Tanzania.

Sowers wakiimba kwenye Tamasha la Saut za Busara mwaka 2010

No comments:

Post a Comment