Home

Sunday, May 8, 2011

Historia ya kundi la Maximum Melodies



Maximum melodies sio kundi geni masikioni mwa watanzania wafuatiliao kwa kina muziki wa injili Afrika Mashariki na kati. Kundi hili lenye maskani yake jijini Nairobi nchini Kenya lilianzishwa mwaka 1997 na vijana waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu ya kimaskini ambao hawakuwa na matumaini na maisha yao ya baadaye. Walianzisha kundi hili wakisaidiwa kwa mambo mengi na Mchungaji wao toka katika kanisa la Maximum Miracle Centre lililo chini ya Pastor Mr & Mrs Muiru ambao nao ni waimbaji. 
Maximum Melodies wakiwa ziarani Nchini Marekani Jimbo la Califonia
Nyimbo yao ya Mwamba mwamba walioifanya chini ya Producer mahiri ajulikanaye kwa jina la Gideoni Kimanzi ndio iliyowapa umaarufu sana na kuwawezesha kufanya ziara sehemu mbali mbali duniani. Nchini Kenya Maximum Melodies wamepata heshima kubwa kufanikiwa kuutangaza vizuri muziki wa Kenya nje ya mipaka ya Kenya.

Andrew young kiongozi wa Maximum Melodies katika mavazi ya Pilot, hii ni wakati wakushoot video ya nyimbo yao iitwayo Manzi ni GOD
 Kulingana na kule Mungu alikowatoa mpaka walipo sasa, wamekuwa wakipata mialiko katika makongamano Mengi ya Vijana kwa minajili ya kuwatia moyo vijana, kuwafundisha kupitia shuhuda zao na kuwaonyesha kuwa Mungu wetu anaweza kumtoa  mtu mavumbini na kumtuketisha pamoja na Wafalme. Katika tuzo zilizomalizika hivi karibuni nchini Kenya za Groove Music Awards, kundi hili lilikuwa moja kati ya Nominees kwenye kategori ya The Best Gospel Group of the Year.

 Ifuatayo ni kazi yao iitwayo Is All About You

No comments:

Post a Comment