Home

Tuesday, May 3, 2011

CBCI Band waandaa Tamasha jijini Mwanza

Kundi Maarufu la kusifu na kuabudu katika jiji la Mwanza lijulikanalo kama CBCI Band toka kanisa la Covenant Bible Church Intenational lililoko nyakato jijini mwanza, Jumapili ijayo tarehe 08/05/2011 wameandaa Tamasha la kusifu na kuabudu litakalofanyika pasipo kiingilio chochote(bure) katika ukumbi wa Vijana Social Hall ulio pembezoni mwa Uwanja wa Ccm Kirumba. 

Akiongeana Hosanna Inc mmoja ya waandaaji wa Tamasha hilo Bro Samuel Nzwalla amesema, tamasha hilo linatarajiwa kuanza mnamo saa tisa kamili jioni mpaka saa kumi na mbili jioni. Pamoja na Kingdom worshipers pia vikundi mbali mbali vya uimbaji vitakuwepo ikiwemo Praise Team toka Saint Augustine University. Kama uko Mwanza huna sababu ya kukosa jumapili hii katika ukumbi wa Vijanna social Hall.

Pamoja na kusifu na kuabudu, CBCI Band watakuwa wakiiweka wakfu album yao ya kwanza yenye nyimbo za kusifu na kuabudu. 

Mch Goodluck Nzwalla Kiongozi wa CBCI Band

No comments:

Post a Comment