Home

Tuesday, May 24, 2011

Omba mvua wakati wa Masika


Uonapo amani kama shwari na usipojua nini kinaumbika katikati ya amani hiyo kwa ajili ya kesho hupelekea kurelax na kuona kila kitu kiko sawa bin sawia.Luka 10:1 Wakati wanafunzi wa kristo walipokuja kwake kwa furaha wakisema Rabi mpaka mapepo yanatutii,ndipo Kristo aliwajibu kwa hekima ya ajabu kulingana na kile alichokua akikiona akasema, Nmemuona shetani akianguka toka juu mpaka chini kama umeme.Maadamu alishuka kama umeme na wao wasijue baada ya kushindwa kwake alikaa vipi akijipanga mara ya pili, ndipo Biblia inatuambia wazi aliporudi uwanjani toka huko alikokuwa ameshuka Petro alishindwa kuhimili ile vita, hata akamkana Masia mara tatu, na Yuda akaishia kumkabidhi Masia mikononi mwa askari wa Pilato.


Uwezo wa kuiona vita yetu kesho pindi unapokua mdogo, ni rahisi sana kutotumia vizuri raslimali tulizonazo leo kwa maana ya mazingira, fedha, muda, cheo, ndugu, marafiki,nk. Wakati kijana baada ya kuhitimu masomo yake na kupata kazi mjini anaweza asione umuhimu wake na badala yake nafasi aliyopata ya kukaa mjini,akaona ni jambo la kawaida tu hivyo tofauti na mshahara anaweza asitengeneze kipato kingine nje ya mshahara wakati mjini nafasi ni nyingi za kufanya hivyo, na mara nyingine anaweza hata asijiendeleze kimasomo kwa kua anavijisababu vilivyomfanya ashindwe kuwaza nje ja ukuta huo. Akili hukaa sawa siku akijikuta kahamishiwa kisiwani Pemba kikazi ndipo anagundua kuwa wakati wa masika hakuutumia vizuri kupanda kwa ajili ya hakiba yake ya keshokutwa.

Wakristo wengi leo ni waombaji wazuri pindi waingiapo matatani, wakati mambo yanaonekana yako shwari huwezi wasikia wakifunga na kuomba ila subiri tatizo litokee ni mabingwa wakushandalai!!. Huwezi wakuta watanzania leo wakimshukuru Mungu kwa amani iliyopo au hali ya chakula iliyopo, ila subiri vyote vipae ndipo tunakutana viwanja vya Jangwani kumsihi Mungu alete hali ya hewa nzuri kwa kilimo au kurejeza amani. Ni nadra sana kumkuta mwanafunzi anasoma kabla test haijatangazwa, na unaweza sikia ooh mimi nikisoma kabla ya test sielewi na hata nikielewa baada ya siku mbili nasahau, ha haaaaa subiri Lecturer atangaze Test uone mahudhurio ya library yanavyokua makubwa na Group discussions zinavyojaa raia!!!.


Kwenye “Wafalme wa Pili” tunaona maisha ya Elisha chini ya Eliya. Umakini wa Elisha katika kujifunza chini ya Eliya ulimfanya Elisha kutotetereka hata baada ya Eliya kuondoka. Kila hatua aliyokuwa akiichukua Eliya lilikuwa ni darasa tosha kwa Elisha. Kwa kuwa ndio ulikuwa wakati wa Masika kwa Elisha, hivyo hakuthubutu kuuchezea alijifunza kila kitu, matokeo yake Elisha alipoingia katika utendaji jamii haikumtofautisha na Eliya.

Unaweza ukapata fursa ya kukaa na dhahabu mikononi mwako kisha usione umuhimu wake mpaka itakapoondoka. Marafiki ulionao, wafanyakazi wenzio, watumishi wa Mungu wanaokuzunguka, ujana, wazazi, na vinginevyo vingi  hizi ni fursa tosha ndio maana Mungu akaviweka karibu nawe. Usipojua kuwatumia kipindi hicho ulichowekwa pamoja nao itakugharimu hapo mbele kwani hutokaa nao Milele, na uko nao kwa kipindi maalumu kwa siku, miezi na miaka iliyoainishwa na Elo-Him. Yule tajiri alipokutana na Lazaro alimsihi Lazaro aende kuwashtua nduguze ili wasiingie pabaya  pasipo mafanikio. Hii ni kwa kuwa alipokuwa duniani hakuiona hiyo fursa ya kukutana na watumishi wa Mungu kisha abadilishe mtazamo.

Mmoja kati ya wachungaji vijana wa Ki-Tanzania ambao kiukweli kwa habari ya ufahamu wa Neno la Mungu wako vizuri ni Pastor Wisdom ambaye kwa sasa yuko Mkoani Kagera na kanisa la Winners Chapel. Aliwahi sema wakati yuko Nigeria zamani haikuwa tabu sana kwake kupata appointment ya kuonana na Prophet Tb Joshua. Mara nyingine walikuwa wanaambiwa Prophert yuko Temple yeyote anaweza kwenda kumuona na sio watu weengi walikuwa wakienda kumuona, Lakini kwa sasa ni ngumu, na Pastor hata akiandika Email kujibiwa huchukuwa Muda, ile access ya kumuona kirahisi haipo tena,


Kwa wanafunzi walioko vyuoni, wanayo fursa ya kuwahubiria wenzao kirahisi mno kuliko baada ya ya miaka mitano ijayo. Ikiwa asiyeokoka uliyenae karibu chuoni anapata Boom na wee unapata, anaishi kibishi kama wengine, kumuhubiria huyu habari za kristo kwa kipindi hiki ni rahisi mno kuliko kumhubiria akiwa tayari ni Regional Manager wa Kampuni fulani hapa mjini.




Mboya V.

No comments:

Post a Comment