Home

Saturday, June 11, 2011

Efraim Sekeleti Abadili jina la Album yake mpya ya Kiswahili

Efraimu Sekeleti
Efraim Sekeleti si jina geni sana kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini Tanzania, ni kijana wa Kizambia ambaye ametamba sana nchini hapa kutokana na nyimbo zake za injili kujizolea maelfu ya mashabiki. Efraimu ambaye ameoa na ana mtoto mmoja, mwaka huu mwanzoni aliiambia Hosanna Inc kuwa album yake mpya kwa Lugha ya kiswahili itaitwa Vigelegele. Ila kutokana na sababu za msingi zaidi ameamua kubadili jina la album hiyo na sasa itaitwa Acha Kulia.

Efraimu ambaye hajui lugha ya kiswahili kwa ufasaha, kwa sasa yuko nchini Uingereza katika jiji la Worshington akifanya huduma. Album hiyo ya ACHA KULIA inatarajia kutoka ndani ya mwaka huu wa 2011. Hosanna Inc itawaletea undani wa album hiyo pindi mambo yakiwa tayari.

No comments:

Post a Comment