Home

Monday, June 27, 2011

Huima Band wafanya Tamasha jijini Mwanza


Kundi kongwe la muziki wa injili jijini Mwanza maarufu kama Huima`s Band lililo chini ya kanisa la FPCT, jumapili ya jana lilifanya Tamasha la kusifu na kuabudu katika ukumbi wa NYUMBANI HOTEL ulio katikati ya jiji la Mwanza. Tamasha hilo la kipekee liliambatana na tukio la kurekodi LIVE video ya album yao mpya. Kazi ya kurekodi video hiyo ilifanywa na kampuni maarufu kwa kazi hizo iitwayo MBC HOTMEDIA.
Huima ni moja kati ya makundi yaliyofanikiwa kuanzisha utaratibu wa kufanya matamasha na kuimba LIVE bila kutumia Playback. Huu ni mwanzo mzuri wa uimbaji uliotukuka kwa utukufu wa MUNGU.
Hapa ilikuwa mida ya sa nane mapema kabisa watu wakianza kuingia na huima wakijipanga tayari kwa shughuli
Kazi ikaanza ilikuwa ni patashika

Huima Band sio muziki tu hata Dressing code walijipanga

Watu waliacha viti, hahaaa Mungu ni mwema kwa wote wamchao

No comments:

Post a Comment