Home

Friday, June 10, 2011

Last Night Campus of Praise and Worship at SAUT 2011

Leo ndio leo katika viunga vya Saint Augustine University Mwanza ambapo wanafunzi waliookoka chini ya Tafes wanafunga mwaka wa masomo wa 2011 kwa Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu.Tamasha hili la aina yake linatarajia kufanyika usiku kucha ambapo Praise and Worship Team toka Tafes Saut pamoja na kundi maarufu jijini Mwanza kwa kusifu na kuabudu lijulikanalo kama Kingdom Worshipers watakuwa wakihudumu kwa pamoja.

Hili ni tamasha kubwa ambalo linafuatia baada ya lile lililowahi kufanyika uwanja wa CCM Kirumba mwaka 2008 na lile lililofanyika  mwezi wa pili mwaka huu katika viwanja vya shule ya msingi Nyamalango iliyo pembeni mwa chuo cha Saut. Kwama uko Mwanza hutakiwi kukosa kwa kuwa Mungu ni ROHO nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli.

Sehemu ya maandalizi ya Tamasha la kusifu na kuabudu lililofanyika Saut mwezi wa Pili mwaka huu

No comments:

Post a Comment