Home

Tuesday, June 7, 2011

Mkristo ahukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la Kushuhudia habari za YESU nchini Algeria

Moja ya Ibada za wakristo nchini Algeria
Siagh Krimo ni mkristo anayeishi nchini Algeria, siku kadhaa zilizopita amehukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kushuhudia habari za Kristo Yesu. Krimo ambaye ana mke na watoto siku moja alipokuwa nyumbani kwake aliamua kuwashuhudia majirani zake habari za kristo. Baada ya kuwashuhudia, majirani hao walienda kumshitaki mahakamani kwa kosa la kumkebehi na kutoa kauli za kumpinga Mtume Muhamad.


Baada ya kesi kusikilizwa hatimaye mahakama ya nchi hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita iliamua kuwa Krimo aende Jela kwa Miaka Mitano kwa kuvunja kifungu cha sheria za nchi hiyo kifungu Namba 144 ibara ya 2 kinachomtia hatihani yeyote anayemkebehi Mtume Muhamad au kuukashifu Uislamu nchini humo.


Hatua hii ya Mahakama ya Algeria anakuja muda mfupi Baada ya mahakama hiyo kuamuru kufungwa kwa makanisa saba yaliyoko katika kitongoji cha Bejaia nchini Humo. Algeria pamoja na kuwa na kipengele cha uhuru wa kuabudu katika katiba yao, lakini kila siku imekuwa ikiweka adhabu kali kwa yeyote ambaye hafuati misingi ya dini ya kiislamu.

Source:Christian Post

1 comment: