Home

Saturday, June 18, 2011

Huima Band Kuzindua Album yao jijini Mwanza


Kundi maarufu jijini Mwanza katika tasnia ya uimbaji liitwalo HUIMA`S BAND, linatarajia kufanya uzinduzi wa Album yao siku ya Tar 26/06/2011 katika ukumbi wa Nyumbani Hotel ulioko katikati ya jiji la Mwanza. Hosanna Inc ilipata nafasi ya kufika kwenye kwenye studio yao iitwayo Melody iliyoko Mwaloni jijini Mwanza na kushuhudia mazoezi maalumu kwa ajili ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa mmoja wa Viongozi wa kundi hilo Bro Fumbuka alisema, lengo kubwa la Tamasha hilo ni kumsifu na kumwabudu Mungu pamoja na kurekodi Video Live siku hiyo. kazi nzima ya kurekodi Live itafanywa na MBC HOT MEDIA ambao wamebobea kwenye kazi hiyo na kila mtu atakayeingia atapewa bure AUDIO CD ya Kundi hilo. HUIMA`S BAND litakuwa ni kundi la Kwanza jijini Mwanza kurekodi Video Live, hizi ni dalili njema za mapinduzi ya Muziki wa injili jijni Mwanza.

Huima Band wakiwa mazoezini tayari kwa tukio la Uzinduzi

Mazoezi yakiendelea

No comments:

Post a Comment