Home

Wednesday, June 8, 2011

Panua mahali pa himaya yako.


Mch Daniel Kulola
Miaka ya nyuma watu wengi  waliookoka  suala lakwenda shule hawakulipa kipaumbele, agenda yao kubwa ilikuwa ni kwenda mginguni.Kwenye upande wa siasa nako hawakujikita huko waliona kama ni dhambi hivyo wakabaki kanisani na hoja ni kwenda mbinguni. Watoto wa mama mdogo wao siasa waliipa kipaumbele na kuona wanaweza kuwa waamuzi katika jamii. Matokeo halisi hali hiyo lleo yako dhahili ndio maana utakuta katika maeneo mengi kuanzia Balozi wa nyumba kumi, Mwenyekiti wa mtaa, katibu kata, Diwani mpaka mbunge wote ni watoto wa mama mdogo(waislamu).


Wakati umefika kwa sisi tunaomjua Mungu tubadilike, Isaya anasema PANUA HEMA, na sisi hatuna budi kupanua mahali pa himaya zetu. Tusiishie kuhubiri tu No!! Lazima tumiliki na uchumi, Tusiishie kuimba kwaya tu No!! lazima tujikite na kwenye siasa na kujiingiza pia kwenye shughuli mbalimbali.Kama uliyeokoka una Diploma usilidhike na kiwango hicho, kuwa na kiu ya kufika mbali zaidi kwenye Digrii ya kwanza, ya Pili mpaka PHD.


Leo hapa nchini mpaka selikali inapanga utaratibu wa watu kwenda Loliondo ni kwa kuwa walioko selikalini wengi hawana hofu ya Mungu. Hivyo wao hawaoni ubaya juu ya hilo, kwao ni sawa tu kwa kuwa huwezi kupata busara kwa mtu asiye na busara.Na kwakufanya hivyo umasikini unazidi kukomaa kwani ufumbuzi wa kudumu wa matatizo ya watu hautoki kwa mwanadamu, bali hutoka kwa Mungu.Ni lazima sasa watu waliookoka na wenye hofu ya Mungu wasome sana na wenye wito wa kujikita kwenye siasa waende huko ili kuleta mabadiliko na hofu ya Mungu ndani selikali.



Mabadiliko siku zote sio suala la siku moja, huchukua muda mrefu, Mwaka 1990 wakati nahubili injili wilayani Geita Mungu aliniambia Daniel nimekuita, sio tu utahubiri hapa Tanzania bali Utahubiri Afrika na Ulimwenguni kote. Baada ya siku kadhaa Mungu akauleta tena ujumbe huo kwangu kwa mara ya Pili. Anachosema Mungu lazima kitimie mwaka 1997 Mungu akadhihilisha ujumbe wake wa mwaka 1990.Nikahubiri Afrika na nchi nyingi Duniani mpaka hivi leo.

Tuliookoka ni Muhimu sana tuamue kuongeza himaya ya mahali petu, tusiridhike na hatua tuliyopo. Hata wale wenye ukoma walisema “Tukibaki hivi tutakufa”, Hawakuridhika na ukoma wao walitaka mabadiliko katika maisha yao. Usipotaka mabadiliko na ukiridhika na hali uliyo nayo huwezi toka kwenye hatua hiyo na kwenda kwenye hatua nyingine.

No comments:

Post a Comment