Home

Monday, June 20, 2011

Uzinduzi wa Album ya MIRIAM LUKINDO Ni Asubuhi Katika Jiji la MWANZA

Mwanamuziki Mahiri wa Nyimbo za Injili Maarufu kama Miriamu Lukindo, jana katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza amefanikiwa kuzindua album yake iitwayo Ni Asubuhi. Uzinduzi huo wa kipekee ulifanyika kwa udhamini Mkubwa wa Haak Neel Production ambao walikuwepo na timu yao nzima kutika Dar es salaam.

Miriamu na Haak Neel Production wamefanikiwa kufanya kile kitu ambacho wengi wa mapromota wameshindwa, kwa Mara ya Kwanza Mwanza Tamasha limefanyika LIVE pasipo Playback. Kwa hili ni pongezi kubwa Miriamu. Miriam alikuja na timu yake ya wapigaji wa vyombo pamoja na watu wa back-vocal toka Dar es salaam na kiukweli walionekana dhahili wamejipanga kwa ajili ya kufanya Live kitu ambacho walifanikiwa.

Katika hali ya kuonekana kama mazoea ya Playback, mara wanamuziki wengine kama Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Neema Mwaipopo walipokuwa wakiimba kwa Playback wakazi wengi wa Mwanza walionekana kurespond kwa kuchangamka, ila Pindi Miriamu na Crew yake walipopanda Jukwaani na Kupiga LIVE. wakazi wa Mwanza walionekana kumshangaa Miriam Kuanzia Vocal Capacity aliyonayo, timu yake ya kumback pamoja na Crew ya wapigaji ambayo kiukweli jamaa walishangaza watu kwa uwezo wao wa kuchezea vyombo. Kwa huu ni Tamasha la kwanza la muziki wa injili kwa Ubora jijini Mwanza.


Kikosi kazi cha Miliamu Kikishuka garini tayari kwa shughuli

Miriam Lukindo akiwa Jukwaani 

Kijitonyama Upendo Group walikuwepo kumsindikiza Miriam

Neema Mwaipopo ha haaaa Raha Jipe Mwenyeweeeeeeeeeeee

Upendo wa Yesu Wanizunguka ilikuwa ni Patashika Upendo Nkone alipopanda Jukwaani

Ilikuwa ni Patashika

Miriam Na Kundi lake wakiwa Jukwaani

Miriam On STAGE, ilidhihirika wazi kuwa huwezi mtenga Miriam na KUABUDU,hapo ilikuwa mwanzoni kabisa mwa tamasha akiimba Amen Amen 
Miriam Lukindo akiimba Ni Asubuhi

Crew ya wapiga Vyombo, wa Kwanza kulia ni Bro Amani ambaye ni MUSIC DIRECTOR Miriam, Miriam anasema ni ngumu yeye kuimba pasipo amani kuweka mambo sawa. Kwenye Drumz anaonekana Bro Kapama akiwajibika

Crew Nzima ya Haak Neel Ikiwajibika

No comments:

Post a Comment