Home

Friday, July 1, 2011

Dj Sooxy wa Kubamba Tv show afunga ndoa na Anne waichigo

Walio katikati ni Dj Sooxy na Mkewe siku ya Harusi yao, pembeni yao ni Dj Moz na Mkewe Debora
Dj sooxy ni mmoja kati ya  Ma Dj watatu wanaounda kundi maararufu la ma DJ waliokoka nchini Kenya liitwalo K-KREW, Kundi hili si geni sana kwa watanzania ambao huangalia CITIZEN TV siku ya jumapili asubuhi, Ma Dj hao Dj Moz Dj John Celeb na Dj Sooxy ambao pia ni watangazaji kwa kushirikiana na mwanadada Kambua ambaye ni muimbaji wa Injili nchini Kenya huendesha vipindi vya RAUKA pamja na KUBAMBA

Dj Sooxy jumapili ya tarehe 18/06/2011 alifunga ndoa na Anne Waichigo, Dj Sooxy  ambaye jina lake kamili ni Jackson Kamau alisindikizwa kwenye tukio hilo na rafiki yake na mwana K-Crew mwenzie Dj Moz na mkewe Debra(mzungu) waliokuwa ndio ma Best wa maharusi hao.

Utamaduni wa kuwa na ma Dj waliokoka hapa Tanzania haupo na ni jambo geni ingawa umuhimu wao upo na hili halina mjadala. Hosanna Inc inaandaa Makala inayohusu Ma Dj walikoka na kazi zao kwa maendeleo ya muziki wa injili kwa kuwa duniani kote hawa watu wapo wakimtumikia Mungu hasa inapokuja kwenye suala la Live Performance na Redioni .Hosanna Inc inawapa hongera maharusi hao kama watenda kazi katika Ufalme wa Mungu.


No comments:

Post a Comment