Home

Monday, July 25, 2011

Ephraim sekeleti kutua nchini mwezi Ujao

Ephraim Sekeleti
Mwanamuziki anayekubalika sana nchini Tanzania akitokeaa nchini Zambia aitwaye Ephraim Sekeleti, anatarajiwa kuja nchini Tanzania mwezi ujao[August]. Sekeleti ambaye nyimbo zake kama Ndani ya Jina, Uniongoze,na Huu Mwaka  zimempa umaarufu sana hapa nchini. 

Sekeleti aliiambia Hosanna Inc ijumaa iliyopita kuwa ujio wake huo utakuwa sambamba na kuitambulisha albium yake mpya iitwayo “Acha Kulia

Sekeleti alizidi kusema kuwa album yake hiyo ambayo mkimsingi ni ya Pili kwa upande wa album zake alizoimba kwa Lugha ya  Kiswahili inajumla ya nyimbo kumi na mbili[12] na Katika nyimbo zote hizo kazifanya akiwa nchini zambia.

Hosanna Inc ilitaka kujua kama kuna wanamuziki wa injili kutoka Tanzania ambao wanajulukana nchini ZAMBIA. Katika kulijibu swali hilo Sekeleti alisema  Zambia wanamjua sana Rose Muhando na wengine kidogo. Mpaka sasa Ephraimu Sekeleti ameshatoa wimbo mmoja uitwao Uniguse Bwana ili kuitambulisha album yake hiyo mpya.

No comments:

Post a Comment