Home

Thursday, July 21, 2011

J Sisters kufanya Uzinduzi Live wakishirikiana na Glorious Celebration


J Sisters
Kundi mahiri la muziki wa kizazi kipya toka familia moja liitwalo J Sisters tar 31/07/2011 katika ukumbi wa Diamond Jubelee wanatarajiwa kuzindua album yao mpya LIVE pasipo Playback kwa ushirikiano mkubwa na Bendi ya Glorious Celebration.
  
Huu utakuwa ni uzinduzi wa aina yake kwa kuwa wanamuziki wengi siku ya uzinduzi huendelea na mazoea ya kufanya Playback Hii itakuwa ni moja kati ya mafanikio ya J sisters katika kwenda katika Level nyingine ya uimbaji na pia  itawaongezea uzoefu kundi la Glorious Band.

Glorious Celebration wakiimba LIVE siku ya utoaji tuzo kwa wanamuziki wa injili nchini Tanzania tukio lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee


No comments:

Post a Comment