Home

Friday, July 8, 2011

J Sisters Kufanya Uzinduzi Wa Album Yao Mpya Diamond Jubelee Tar 31/7/2011

J Sisters

Kundi maarufu la muziki wa injili nchini Tanzania linaloundwa na mabinti wanne ambao wote ni ndugu wa familia moja liitwalo J sisters, tarehe 31/06/2011 litakuwa likifanya uzinduzi wa album yao katika ukumbi wa Diamond Jubelee.
                      
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi kundi hilo litakuwa likisindikizwa na waimbaji mashuhuli chini hapa ambao baadhi yao wanaabudu pamoja na kundi hilo katika kanisa la Eagt Mito ya Baraka lililoko maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam.

Mabinti wawili wakubwa wanaounda kundi hilo toka familia ya Mshama wanasoma masomo ya juu nchini Marekani katika chuo kikuu cha Liberty, kwa sasa wako likizo wakati wawili wadogo wanasoma hapa nchini. Hii itakuwa ni album ya tatu kwao baada ya album zao mbili walizozifanya siku za nyuma

J Sisters wakiwa katika viwanja vya Jangwani wiki mbili zilizopita wakati wa mkutano wa Injili wa Askofu Moses Kulola jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment