Home

Wednesday, July 27, 2011

Mch Danel Kulola na Masanja mkandamizaji waiteka wilaya ya Nzega kwa injili


Mch Daniel Kulola akiwa na Masanja Mkandamizaji
Kwa Takribani wiki moja Mtumishi wa Mungu Daniel kulola akiwa pamoja na Msanii maarufu nchini Kutoka kundi la Ze Comedy Masanja Mkandamizaji  waliiteka wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwa Injili ya Yesu Kristo.

Katika mkutano huo uliomalizika jumapili iliyopita Mch Daniel Kulola ndiye aliyekuwa akihubiri injili na huku msanii Masanja ambaye kwa sasa ameokoka alikuwa akiimba na kufanya comedy zilizowavuTa watu wengi wafike kwenye mkutano huo na hatimaye kumpokea kristo.

Hosanna Inc ilifanikiwa kuongea na Mch Daniel kulola wakati wakiwa wilayani hapo na akaiambia kuwa Kazi iliyofanyika Nzega ni Kubwa na watu wengi walimpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yao.

Hii ni approach mpya kufanywa na kanisa katika kuwavuta watu wengi wafike kusikiliza Neno la Mungu, kwa kuwa kwa miaka ya hivi karibuni watu wengi wamekuwa hawana muitikio mzuri wa kuhudhuria kwenye mikutano ya Injili.

No comments:

Post a Comment