Home

Friday, August 12, 2011

Monalisa na mamaye{Natasha} wabatizwa

Mcheza Filamu na maigizo maarufu nchini Tanzania Yvonne Cherri ambaye wengi wanamtambua  kwa jina la Monalisa,  pamoja na mama yake mzazi ambaye nayee ni muigizaji Susane Lewis { Natasha}, siku za hivi Karibuni walibatizwa ubatizo wa maji Mengi baada ya kuokoka na kufundishwa  kutimiza kweli yote katika kanisa la Blessing  Church lililopo Kongowe nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Yvonne Cherry Monalisa (Mwenye Miwani)
Kanisa hilo lililoko chini ya Mtumishi wa Mungu Mtume David na Marry Lutumba  lina utaratibu maalumu ambapo watu waliookoka baada ya kufundishwa  namna ya kukulia wokovu na umuhimu wa ubatizo hatimaye hubatizwa kanisani hapo.

Monalisa ambaye ameokoka zamani na alimtamgulia mamaye kokoka , amekuwa akisali kanisani hapo kwa muda mrefu sasa na amewahi kukiri juu ya ukweli  wa wokovu wake kupitia interview aliyofanya siku za Nyuma katika kipindi cha Bongo Movie kinachoendeshwa na Mwanadada Joyce Kiria katka kituo cha Television cha Channel Five.

Monalisa kushoto akiwa na mama yake(Natasha) Kulia
Ni matumaini yetu kuwa kanisa{watu waliookoka}  litafanya juhudi za dhati katika kuwalea na kuwakuza watumishi hawa katika  safari yao ya wokovu. Kanisa linapaswa kukumbuka kuwa  hadi kufikia Mungu  kuwaokoa watu hawa, ina maana kuna wajibu amewapa wa kuufanya ndani ya kanisa. 

Hivyo kanisa lazima lisimamie kuhakikisha kuwa ule utumishi uliowekwa ndani yao kwa utukufu wa Mungu unakuwa dhahiri{ Material} katika mwili na katika Roho pia.

1 comment:

  1. god has a mission and purpose to his people, he statred with k-basil, then q jay (bongo flavour to gospel songs),Masanja, now MOnalisa and her mother, God never fail, we expect more great names in the kingdom of living GOD.
    keep on praying for WEMA SEPETU also

    ReplyDelete