Home

Tuesday, August 2, 2011

Uzinduzi wa album ya J sisters


J sisters ni kundi la Muziki wa injili linaloundwa na na Mabinti watatu kutoka katika familia moja ya Mr Mshama. Jumapili iliyopita kundi hilo liliweza kufanikiwa kuzindua album yao mpya katika ukumbi wa Diamond Jubelee.

Uzinduzi huo wa aina yake ulifanywa LIVE na vijana hao kwa ushirikiano Mkubwa wa Bendi ya Glorious Celebration ya Jijini Dar es salaam chini ya Bro Emmanuel Mabisa na Bro Sanga. Miongoni mwa wanamuziki wakubwa waliosindikiza uzinduzi huo ni Pamoja na Flora Mbasha, Anastazia Mukabwa, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja  pamoja na Kundi zima la Glorious Celebration.

J sisters Wakiwa On stage

Mama mzazi wa vijana hao akiongea siku ya uzinduzi huo

Glorious Band wakiimba siku hiyo

No comments:

Post a Comment