Home

Saturday, September 3, 2011

Mwl Christopher Mwakasege Kuanza Semina Biafra kesho


Mwl C.Mwakasege na mama Diana Mwakasege wakifanya maombezi katika moja ya Semina zinazoendeshwa na Huduma ya Mana
Mwalimu Christopher Mwakasege  kutoka Arusha ambaye anaongoza Huduma ya MANA, Kesho tarehe 4/09/2011 kuanzia saa Tisa mchana katika Viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam anatarajia kuanza Semina ya Neno La Mungu ambayo ni mahususi kwa watu wote.

Hosanna Inc tunampa pole Mwl Mwakasege kwa kufiwa na Baba yake mzazi mwezi uliopita mwishoni kitendo ambacho kilipelekea Semina ya Mwl Mwakasege iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 27-28/08/2011 katika jiji la Birmingham nchini Uingereza kuahirishwa.

Hii ni Fursa tena kwa wakazi wa Dar es salaam Kula Mana ili wakue Kiroho kwa kuwa Dar es salaam ni moja kati ya mikoa yenye Neema ambapo Mwl Mwakasege hufanya semina zaidi ya Mara moja kwa mwaka .

No comments:

Post a Comment